IQNA

Misri imejenga misikiti mipya 1000

16:15 - November 11, 2015
Habari ID: 3447288
Waziri wa Awqaf nchini Misri ametangaza kuwa misikiti mipya zaidi ya 1000 imejengwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa tovuti ya el-balad.com, Muhammad Mukhtar Gomaa amesema wizara hiyo binafsi imechangia ujenzi wa misikiti 779.
Akizungumza katika ufunguzi wa Chuo Kikuu cha Cairo amesema kuwa himaya hii haina kifani katika historia ya ujenzi wa misikiti Misri na nchi za Mashariki ya Kati.
Huku akibainisha nafasi ya Msikiti Mkuu wa Jamaa katika Uislamu na athari zake miongoni mwa Waislamu, amesema wizara yake iko tayari kuwaajiri wahubiri vijana wawe maimamu katika misikiti hiyo.
Amesema kuajiriwa maimamu vijana ni njia muafaka ya kuwavutia vijana misikitini na kuwazuia kujiunga na makundi yenye misimamo mikali ya kidini na wakufurishaji.

3444838

captcha