IQNA

Serikali ya Sudan kusaidia Madrassah za Qur'ani

19:34 - May 05, 2017
Habari ID: 3470968
TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Sudan imesema inaunga mkono Madrassah za jadi za nchi hiyo zinazofunza Qur'ani Tukufu.
Makamu wa Rais wa Sudan Mohammad Abdulrahman ameyasema hayo Alhamisi wakati alipokutana na Sheikh Dafiullah Bakhit, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Qur'ani Tukufu nchini humo.
Katika kikao hicho, afisa amesisitiza kuwa serikali ya Sudan inalipa uzito mkubwa na ina hamu ya kuunga mkono Madrassah za jadi za Qur'ani maarufu kama Khalawi.
Ameongeza kuwa serikali inaunga mkono Khalawi kwa sababu zina nafasi muhimu katika kutoa mafundisho ya Qur'ani na pia katika kuwawezesha vijana wahifadhi Qur'ani Tukufu.
Kwa uapnde wake  Sheikh Bakhit amesema katika kikao hicho wamejadili nafasi ya Jumuiya ya Qur'ani nchini Sudan sambamba na kuimarisha mbinu za kufunza Qur'ani Tukufu. Aimesema pia wamejadili njia za kuinua kiwango cha Khalawi katika jamii ya watu wa Sudan.
3596262
captcha