IQNA

Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sudan yaanza

10:58 - January 09, 2018
Habari ID: 3471348
TEHRAN (IQNA)-Fainali ya Mashindano ya Tisa ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Sudan imeanza Jumanne hii katika mji mkuu, Khartoum.

Siku ya Jumapili na Jumatatu kulifanyika mchujo ambapo waliofuzu waliingia katika mashindano ya fainali ambayo yataendelea hadi Jumamosi Januari 13.

Kuna jumla ya washiriki 73 waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi 50 ambao wamefika mjini Khartoum kushiriki katika mashindano hayo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawakilishwa katika mashindano hayo na Hafidh Mohammad Rasul Takbiri.

Kwa mujibu wa Maaz Fatih al-Hajj, mmoja kati ya wasimamizi wa mashindano hayo,  maarufu kama Zawadi ya Khartoum, washiriki wanashindana katika vitengo viwili tafauti vya wanawake na wanaume.

Ameongeza kuwa, pembizoni mwa mashindano hayo kuna semina kadhaa pamoja na hafla za kiutamaduni. Aidha kutakuwa na mihadhara kuhusu miujiza ya Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW na kati ya watakaohutubu ni mwanazuoni mashuhuri wa Misri Sheikh Omar Abdul Kafi Shihatta.

3680052

captcha