IQNA

Magaidi 200 wa Al Shabab wafikishwa mahakamani Msumbuji

8:41 - October 05, 2018
Habari ID: 3471702
TEHRAN (IQNA)-Maafisa wa mahaka za Msumbiji wametangaza kuwa wamewahukumu wanachama 200 wa kundi la al Shabab la magaidi wakufurishaji.

Maafisa hao wamesema kuwa, mahabusu 200 wanaotuhumia kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la al Shabab waliokuwa wakihusika na vitendo vya kigaidi na kuzusha ghasia katika maeno yenye utajiri wa mafuta ya kaskazini mwa nchi hiyo wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Ripoti zinasema kuwa, 50 kati ya watuhumiwa hao ambao walitokea nchi jirani ya Tanzania wamehukumiwa katika gereza ya mkoa wa Cabo Delgado. Vijiji vya mkoa huo ulioko kaskazini mwa Msumbiji vimekuwa vikisumbuliwa na mashambulizi ya umwagaji damu ya wanachama wa kundi la al Shabab tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2017.
Ripoti ya serikali ya Msumbiji inasema wapiganaji wa kundi la al Shabab wameua raia 50 wa nchi hiyo, wakachoma moto vijiji kadhaa na kuwalazimisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.
Kwa sasa serikali ya Msumbiji imetuma askari na polisi katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Tanzania na tayari imewakamata mamia ya washukiwa.
Mwaka uliopita Bunge la Msumbiji lilipasisha sheria inayozidisha adhabu dhidi ya magaidi kufuatia ongezeko la hujuma za kigaidi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

3752587

captcha