IQNA

Waislamu Ohio Marekani wajitahidi kueneza ufahamu wa Uislamu

21:35 - October 08, 2018
Habari ID: 3471703
TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika jimbo la Ohio nchini Marekani wameanzisha mkakati maalmu wa kuhakikisha kuwa wakaazi wote wa eneo hilo wanapata ufahamu sahihi kuhusu Uislamu.

Jumuiya ya Kiislamu ya Miami Valley jimboni Ohio imesema imeanzisha mkakati wake kwa kuwafunza wakaazi wa mtaa wa Springfield kuhusu mafundisho sahihi ya Uislamu.

Hafla hiyo imepangwa kufanyika Jumamosi Oktoba 13 katika Ukumbzi wa Bayley katika Chuo Kikuu cha Wittenburg na watu wote wamakaribishwa kuhudhuria.

Siku ya Kiislamu Ohio imekuwa ikifanyika katika Jumamosi ya pili mwezi Oktoba kwa miaka 31 kabla ya kusimamishwa mwaka 1997 kutokana na kuenea chuki dhidi ya Uislamu. Mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 yalishadidisha zaidi vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani.

3466925

captcha