IQNA

Mtoto Mpalestina wa miaka 8 ahifadhi Qur'ani kamili baada ya miezi 8

16:27 - January 12, 2019
Habari ID: 3471803
TEHRAN (IQNA)- Mtoto mvulana wa Kipalestina mwenye umri minane amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu miezi minane tu baada ya kuanza zoezi la kuhifadhi.

Kwa mujibu wa taarifa, Ali Ivaz ambaye anaishi katika Ukanda wa Ghaza alianza kuhifadhi Qur'ani katika madrassa ya Msikiti wa al Amri mjini Jabalia kaskazini mwa Mji wa Ghaza.

Ali alianza kuhifadhi ukurasa moja wa Qur'ani kwa siku sambamba na kusikiliza sauti za wasomaji maarufu wa Qur'ani. Kwa taratibu alianza kuongeza idadi ya kurasa alizokuwa akihifadhi hadi kufika kurasa 16 kwa siku. Aidha alikuwa akisoma jumla ya kurasa 45 kila siku kabla ya kufanikiwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu. Kwa ujumla ilimchukua muda wa miezi minane kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na hiyo imetajwa kuwa ni rekodi mpya katika Ukanda wa Ghaza.,

Harakati za Qur'ani ni mashuhuri sana katika Ukanda wa Ghaza pamoja na kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita liko chini ya mzingiro ya kinyama wa utawala haramu wa Israel ambao pia umelishambulia eneo hilo kijeshi mara kadhaa.

3780244

captcha