IQNA

Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa herufi za Kiarabu za Borno yazinduliwa Nigeria

10:46 - May 16, 2019
Habari ID: 3471960
TEHRAN (IQNA) – Nakala ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa herufi za Kiarabu za Borno imezinduliwa nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, uzinduzi huo umuhudhuriwa maafisa wa kieneo, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Nigeria na mabalozi wa nchi kadhaa za Kiiskamu akiwemo Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wazungumzaji katika hafla hiyo wamesisitiza umuhimu kwa kuchapisha na kusambaza Qur'ani Tukufu.

Borno, ni herufi za Kiarabu ambazo zimepewa jina la Jimbo la Borno la kaskazini mashariki mwa Nigeria na ni heruf ambazo zilikuwa zikitumiwa kwa karne nyingi na wenyeji wa eneo hilo kuandika Qur'ani Tukufu kabla ya kuacha kutumiwa miongo ya hivi karibuni.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na jitihada za kuhuisha herufi maalumu za Kiarabu za nchi kama vile Pakistan,Misri, Sudan, Senegal, Morocco na Chad.  

captcha