IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Wizara ya Wakfu ya Misri inaandaa vipindi vya Qur'ani Tukufu katika Mwezi wa Ramadhani

21:26 - January 11, 2023
Habari ID: 3476388
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu ya Misri imesema imetayarisha programu mbalimbali za Qur’ani Tukufu na za kidini kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Abdullah Hassan, msemaji wa wizara hiyo alisema kutakuwa na programu na shughuli nyingi katika mwezi mtukufu mwaka huu.

Kutakuwa na duru za usomaji wa Qur'ani Tukufu kwa ushiriki wa wasomaji mashuhuri katika majimbo mbalimbali ya Misri, alisema.

Hassan aliongeza kuwa misikiti mikubwa pia itatayarishwa na wizara kwa ajili ya kuandaa sherehe za Itikaf.

Usambazaji wa vikapu vya chakula miongoni mwa wale wanaohitaji pia ni katika ajenda ya wizara ya Wakfu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, alisema, akibainisha kuwa itakuwa na umuhimu zaidi mwaka huu kuliko miaka iliyopita kutokana na hali ngumu ya kiuchumi nchini humo.

Kwingineko katika maelezo yake, Hassan alisema mashindano ya 29 ya kimataifa ya Qur'ani ya Misri yataandaliwa na wizara hiyo mwezi Februari.

Cairo itakuwa mwenyeji wa hafla hiyo ya kimataifa katika kategoria kadhaa kama vile usomaji wa Qur'ani Tukufu , kuhifadhi, na sayansi ya Qur'ani Tukufu.

 

4113374

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu misri
captcha