IQNA

Waislamu Warohingya

Indhari ya Al-Azhar kuhusu Warohingya kukumbwa na maafa ya kibinadamu

21:27 - February 22, 2023
Habari ID: 3476607
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar ya Misri kimeonya kuhusu mgogoro wa kibinadamu unaotarajiwa kuwakumba wakimbizi wa jamii ya Rohingya iwapo misaada itapungua.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Misimamo Mikali kilisema Shirika la Mpango wa Chakula Duniani linapanga kupunguza msaada wake wa chakula kwa wakimbizi wa Rogingya katika eneo la Cox's Bazar nchini Bangladesh.

WFP imeongeza kuwa WFP itapunguza thamani ya msaada wake wa chakula hadi dola 10 kwa kila mtu kutoka dola 12 kuanzia mwezi ujao.

WFP ilisema inalazimika kupunguza msaada wake wa kuokoa maisha kwa Warohingya wote wanaoishi katika kambi za Cox's Bazar, Bangladesh, kuanzia Machi 1.

Wataalamu wameonya kuwa hatua hiyo itakuwa na madhara makubwa kwa mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wanaoishi katika kambi nchini Bangladesh.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Misimamo Mikali cha Al-Azhar kilizikumbusha nchi za dunia mateso ya takriban watu milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh, na kubainisha kwamba wamekuwa wakikabiliwa na masaibu ya aina mbalimbali katika kipindi cha miaka 6 iliyopita.

Tofauti na makundi mengine yaliyo hatarini, Warohingya wana fursa ndogo za ajira katika kambi nchini Bangladesh, wakitegemea takriban misaada ya kibinadamu kukidhi mahitaji yao ya chakula na mengine muhimu.

Kwa msaada wa wafadhili na washirika, WFP imekuwa ikitoa chakula, lishe na misaada mingine muhimu kwa wanaume, wanawake na watoto wa Rohingya tangu kuhama kwao kutoka Myanmar mwaka 2017.

Licha ya juhudi za pamoja za kibinadamu, asilimia 45 ya familia za Rohingya hazili chakula cha kutosha na utapiamlo umeenea katika kambi hizo.

Warohingya ni jamii Waislamu kutoka kutoka nchi ya Kibudhha ya Myanmar, ambako wamekuwa wakikandamizwa kwa muda mrefu.

Tangu ukandamizaji wa jeshi la Myanmar mwaka 2017, karibu milioni moja wamelazimishwa kuingia Bangladesh huku wengine wakikimbilia nchi zingine za karibu na maeneo mengine duniani.

4123615

Kishikizo: rohingya waislamu
captcha