IQNA

Maafa

Watu 85 waaga dunia katika mkanyagano wakati wakipokea msaada nchini Yemen

21:40 - April 20, 2023
Habari ID: 3476895
TEHRAN (IQNA)- Makumi ya watu wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa huko Yemen katika mkanyagano uliotokea leo katika zoezi la ugavi wa msaada wa hisani.

Mkanyagano huo umetokea leo katika nchi maskini ya Kiarabu ya Yemen siku moja kabla ya Waislamu duniani kusherehekea Sikukuu ya Idul-Fitr baada ya kukamilisha funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Habari zinasema kuwa mamia ya watu walikusanyika leo katika shule moja mjini Sana'a, mji mkuu wa Yemen, kwa ajili ya kupokea msaada wa fedha wa Riali 5,000 za Yemen sawa na dola 8 za Marekani.  

Watu wasiopungua 85 wamepoteza maisha na zaidi ya 322 wamejeruhiwa katika mkanyagano uliotokea kwenye zoezi hilo la hisani katika wilaya ya Babul Yemen huko Sana'a. Wanawake na watoto ni miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo. Wizara ya Afya ya Yemen imeripoti kuwa, watu waliohusika na tukio hilo wamekamatwa. 

Televisheni ya al Masira imeonyesha miili ya watu waliopoteza maisha ikiwa imerundikana katika eneo la tukio. Askari wenye silaha waliovalia mavazi ya kijeshi na wafanyakazi waliokuwa wakigawa fedha hizo za msaada walijaribu kupiga kelele mbele ya umati wa wananchi ili warudi  nyuma ili kuzua msongamano lakini jitihada zao ziliaambulia patupu. 

Muhammad Al al Houthi Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema kuwa idadi kubwa ya watu ndio iliyosababisha mkanyagano katika zoezi hilo la hisani la ugawaji fedha lililosababisha kupoteza maisha watu zaidi ya 80.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen amelaumu kutokuwepo mpangilio mzuri katika ugawaji wa msaada huo.  

Yemen ambayo ni nchi masiini zaidi katika bara Arabu imekuwa ikikabiwa na mashambulizi ya mambomu ya muungano vamizi unaaongozwa na Saudi Arabia tangu mwaka 2015. Hivi karibuni Saudia ilitangaza azma ya kusitisha vita dhidi ya Yemen baada ya kushindwa kufikia malengo yake ya kuiondoa madarakani harakati ya Ansarullah. 

Vita vya Saudia dhidi ya Yemen vimesababisha maafa makubwa na kuwaacha mamilioni nchini humo katika dimbwi la umasikini.

4135630

Kishikizo: yemen saudi arabia
captcha