IQNA

Uungaji mkono kwa Palestina katika ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Kuwait

10:36 - November 09, 2023
Habari ID: 3477866
KUWAIT CITY (IQNA) - Waziri wa Wakfu na masuala ya Kiislamu wa Kuwait amesisitiza haja ya Waislamu kuwaunga mkono watu wa Palestina.

"Hatutasahau kamwe ardhi iliyobarikiwa (ya Palestina) ambapo Mtume wa mwisho, Muhammad (SAW) alipaa mbinguni," Abdulrahman Al-Mutairi alisema, akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa mashindano ya 12 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Kuwait siku ya Jumatano.

Amesikitishwa na mauaji yanayotekelezwa na Israel dhidi ya "ndugu zetu katika imani" katika Ukanda wa Gaza na kwingineko huko Palestina, akisema ukatili unaofanywa na Wazayuni umefikia hatua isiyoelezeka.

Ameongeza kuwa, suala la Quds Tukufu (Jerusalem) si suala la Palestina pekee bali ni suala linalohusiana na ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza kuwa, taifa la Kuwait na pia serikali ya nchi hiyo daima imekuwa ikiwasimamia Wapalestina na kuwaunga mkono.

Kwingineko katika matamshi yake, al-Mutairi ameashiria msisitizo uliowekwa katika shughuli za Qur'ani nchini Kuwait na kusema, tuzo ya kimataifa ya Qur'ani ya nchi hiyo imekuwa na mabadiliko ya kiutamaduni na mafanikio ya kimataifa.

Amewashukuru waandaaji wa mashindano hayo na kusema Kuwait inatilia maanani sana uendelezaji wa usomaji wa Qur'ani Tukufu na kuhifadhi na kuendeleza mafundisho na maadili yake.

Wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali wanashiriki katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani, itakayoendelea hadi tarehe 15 Novemba.

Washindani wanashindana katika kategoria tano zinazojumuisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu, usomaji na Tajweed katika viwango tofauti.

Pia kuna kategoria ambayo mradi bora zaidi unaohudumia Qur'ani Tukufu utachaguliwa na kutunukiwa.

Mashindano hayo yanafanyika chini ya uangalizi wa Emir Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, mtawala wa Kuwait.

Iran ina wawakilishi watatu katika shindano hilo: Amin Abdi katika usomaji wa Qur'ani, Milad Asheghi katika kuhifadhi Quran nzima kwa watu wazima, na Abolfazl Mirabi katika kuhifadhi  Qur'ani kwa watoto.

Support for Palestine Underlined at Kuwait Intl Quran Contest Opening Ceremony

Support for Palestine Underlined at Kuwait Intl Quran Contest Opening Ceremony

3485938

captcha