IQNA

Waislamu Uingereza

Mbunge aliyetoa tamko la chuki dhidi ya Uislamu Uingereza asimamishwa kazi

6:26 - February 26, 2024
Habari ID: 3478415
IQNA - Chama tawala cha Wahafidhina (Conservative) nchini Uingereza kimemsimamisha kazi mmoja wa wabunge wake kufuatia maoni ya chuki dhidi ya Uislamu dhidi ya meya wa London.

Mbunge Lee Anderson hivi majuzi alisema meya wa London, Sadiq Khan, alikuwa alikuwa ametekwa na watu wenye misiamo mikali ya Kiislamu

Khan, Mwislamu wa kwanza kuwa meya wa London na mwanachama wa Chama cha upinzani cha Labour, analengwa mara kwa mara na Wahafidhina kwa jinsi anavyoshughulikia masuala ya polisi katika mji mkuu wa Uingereza, ikiwa ni pamoja na maandamano ya mara kwa mara ya watetezi wa ukombozi wa Palestina.

Siku ya Jumatano mamia ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina walikusanyika nje ya bunge, wakati wa upigaji kura wenye mtafaruku wa kutaka kusitishwa kwa vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Akizungumza siku ya Ijumaa kwa kituo cha televisheni cha GB News, Anderson alisema, "Siamini kabisa kwamba Waislamu hawa wamechukua udhibiti wa nchi yetu. Lakini ninachoamini ni kwamba wanamdhiti Khan na wana udhibiti wa London. Kwa kweli ameukabidhi mji mkuu wetu kwa wenzake."

Matamshi yake yalisababisha ukosoaji mwingi kutoka, huku mwenyekiti wa Chama cha Labour Anneliese Dodds akisema ni matamshi ya "mbaguzi wa rangi na ni chuki dhidi ya Uislamu".

Waziri wa biashara wa kihafidhina Nus Ghani, mbung mwandamizi Sajid Javid na mwenzake wa Tory Gavin Barwell walikuwa miongoni mwa wanasiasa wa Tory waliojiunga na malalamiko hayo, huku Barwell akiyaita maoni hayo kuwa "kashfa mbaya".

Baraza la Waislamu la Uingereza lililaani matamshi hayo na kusema ni ya kuchukiza na yanayoashiria  msimamo mkali.

Khan aliwaambia waandishi wa habari kwamba anachukulia maoni ya Anderson kama ya kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu na kwamba "yatamwaga mafuta kwenye moto wa chuki dhidi ya Waislamu".

Huku kukiwa na ukosoaji mkubwa wa matamshi ya Anderson siku ya Jumamosi, Chama cha Conservative kilisema kimeamua kuwa hawezi tena kukiwawakilisha katika Bunge.

Msemaji wa Simon Hart, waziri wa serikali anayehusika na nidhamu ya chama, ametangaza kuwa: "Kufuatia kukataa kwake kuomba msamaha kwa maoni aliyoyatoa, Mnadhimu Mkuu amemsimamisha kazi Lee Anderson"

Kuanzia sasa ataketi kama mbunge huru bungeni.

Sayeeda Warsi, mjumbe wa Conservative wa Bunge la Malodi na mwenyekiti mwenza wa zamani wa chama hicho, aliwahi kusema waliowengi katika chama chake 'wanauchukia Uislamu kitaasisi".

Maoni ya Anderson yanakuja huku matukio ya chuki dhidi ya Uislamu yakiongezeka kwa kasi nchini Uingereza.

Siku ya Alhamisi taasisi moja ilitangaza kuwa Idadi kubwa ya matukio ya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu yameripotiwa nchini Uingereza tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Gaza, kulingana na kundi linalofuatilia visa kama hivyo.

Taasisi ya Tell MAMA, ambayo hufuatilia taarifa za chuki dhidi ya Uislamu, imesema ilirekodi matukio ya chuki dhidi ya Uislamu yapatayo 2,010 kati ya Oktoba 7, 2023 na Februari 7, 2024. Hiyo ilikuwa zaidi ya mara tatu ya matukio 600 yaliyorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka uliotangulia, ongezeko la asilimia 335.

3487328

captcha