Mahfel ni kipindi maalum cha Runinga cha Ramadhani. Onyesho la msimu wa pili wa kipindi hicho maarufu lilianza kwenye chaneli ya 3 ya IRIB katika siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mnamo Machi 12.
Katika kipindi kilichorushwa hewani siku ya Ijumaa, Machi 29, 2024, Karim Mansouri alisoma aya za 78-82 za Surah Ash-Shu'ara pamoja na aya za 1-15 za Surah Ash-Shams.
Kipindi hicho hutangazwa kabla ya Magharibi kila siku katika mwezi mtukufu, na kuwapa watazamaji hali nzuri ya kiroho wanapojitayarisha kufuturu.
Kwa kuzingatia Qur'ani, kindi hiki kinalenga kuwapa watu waliofunga muda mfupi wa kunufaika na mijadala yenye utambuzi na usomaji wenye kuvutia wa Qur'ani Tukufu.
https://iqna.ir/en/news/3487749