IQNA

Hija na Umrah

Saudia yafafanua masharti ya Visa ya Umra kabla ya Hija

20:06 - April 20, 2024
Habari ID: 3478705
IQNA – Serikali ya Saudi Arabia imefafanua masharti ya viza ya Umra, ikibainisha kuwa wote wanaoshiriki katika ibada ya Hija ndogo ya Umra wanapaswa kuondoka nchini humo huo kufikia Juni 6.

Wizara ya Hija na Umra nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa Dhul Qadah tarehe 29, 1445 (Juni 6), itakuwa siku ya mwisho kwa wenye visa ya Umra kuondoka katika Ufalme huo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Hija.

Wizara hiyo ilisema kuwa visa ya Umra kwa  ina uhalali wa siku 90 kutoka tarehe ya kuingia Saudi Arabia.

Ufafanuzi huo ulikuja kutokana na maswali mengi yaliyopokelewa kupitia akaunti ya wizara kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Tangazo hilo linafuatia ripoti za awali zilizosema Dhul Qadah 15, 1445, kama tarehe ya mwisho kwa wenye viza ya Umrah kuingia Saudi Arabia mwaka huu.

Wizara pia ilisisitiza kuwa muda wa visa ya Umra hautaongezwa zaidi ya siku 90 na haiwezi kubadilishwa kuwa aina nyingine ya visa.

Maombi ya viza ya Umrah yanaweza kufanywa kupitia mifumo ya kielektroniki iliyoidhinishwa ya huduma za Umra, inayopatikana katika https://nusuk.sa/ar/partners

Hatua hii imekusudiwa kuhakikisha mtiririko mzuri na wa utaratibu wa Mahujaji katika miji mitakatifu ya Hija.

3487996

Kishikizo: hija umrah 1445 saudia
captcha