IQNA

Algeria ina wanafunzi milioni moja wanaosoma Qur'ani

13:49 - October 20, 2019
Habari ID: 3472181
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini nchini Algeria amesema takribani wanafunzi milioni moja wanasoma wanaosoma Qur'ani katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Yusuf Bilmahdi, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini ameongeza kuwa serikali ya Algeria inalenga kuimarisha masomo ya Qur'ani katika nchi hiyo ya Kiislamu.

Waziri Bilmahdi amebaini kuwa masomo maalumu ya Qur'ani yanatolewa sambamba na masomo mengine rasmi katika shule na vyuo vikuu nchini Algeria.

Waziri wa Wakfu Algeria ameyasema hayo wakati wa kufunguliwa Sheule ya Qur'ani ya Dararia nje kidogo ya mji mkuu, Algeria siku chache zilizopita. Waziri Bilmahdi pia alifungua Msikiti wa Salman Farsi na kituo chake cha Qur'ani katika eneo la Bab Ezzouar mtaandi Dar Elbeida nje kidogo ya Algiers.

Nchi ya Algeria inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 42 ambapo asilimia 98 ni Waislamu.

3850413

captcha