Waziri wa Uchumi Airlangga Hartarto, ambaye anasimamia mpango wa kitaifa wa kukabiliana na COVID-19 na kuhuisha uchumi amesema serikali ya Indonesia inalenga kupata dozi milioni 320 za chanjo ya COVID-19.
Amesema serikali imeshauriana na Baraza la Maulamaa Indonesia ili kuhakikisha kuwa chanjo hiyo inapata cheti cha ‘Halal’.
Raia wengi wa Indonesia wamekuwa na wasi wasi kuwa yamkini chanjo cha COVID-19 ikawa na mada ambazo ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Maafisa wa serikali ya Indonesia wanatazamiwa kuitembelea China kuchunguza mchakato wa utegenejzai chanjo ya COVID-19 ili kuhakikisha kuwa haikiuki mafundisho ya Kiislamu.
Hadi sasa watu zaidi ya laki tatu 337,000 wameambukizwa COVID-19 Indonesia na miongoni mwao wengine karibu 12,000.