IQNA

Saudia yatangaza wamu ya Pili ya Ibada ya Umrah

15:53 - October 13, 2020
Habari ID: 3473255
Wizara ya Hija na Umrah Saudia imetangaza kuwa watu 250,000 wataruhusiwa kushiriki katika awamu ya pili ya Ibada ya Umrah ikiwa ni katika mpango wa kuanza hatua kwa hatua ibada hiyo.

Taarifa ya wizara hiyo imesema duru ya pili ya Umrah itaanza Oktoba 18 na duru ya tatu, ambayo itawajumuisha wageni kutoka nje ya Saudia itaanza Novemba 1.

Taarifa hiyo imesema kila nchi itapangiwa idadi maalumu ya raia wake wanaoweza kushiriki katika umrah.

Saudia ilipiga marufuku Ibada ya Umrah zaidi ya miezi sita iliyopita baada ya kuibuka janga la corona. Mwaka huu pia kutokana na corona, ni idadi ndogo sana ya Waislamu walioweza kutekeleza ibada ya Hija na wote walikuwa ni wakaazi wa Saudia.

Utawala wa Saudia umekuwa ukikoslewa kwa kutozihusisha nchi za Kiislamu dunaini katika maamuzi yake kuhusu ibada za Hija na Umrah. Hatua ya Saudia ya kujichukulia maamuzi ya upande mmoja pia imekosoelwa na maulamaa wa Kiislamu dunaini.

Msomi na mhadhiri wa chuo kikuu nchini Kuwait miezi michache iliyopita aliibua utata katika mitandao ya kijamii baada ya kusema hatua ya Saudia wa kupunguza idadi ya mahujaji mwaka huu itaubadilisha Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid al Haram, kuwa sawa na jumba la makumbusho.

Hakim al-Mutairi mhadhiri wa Tafsiri ya Qur’ani Tukufu na Hadithi katika Chuo Kikuu cha Kuwait amekasirishwa na uamuzi wa Saudia wa kuwazuia mahujaji kutoka nje ya Saudia kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu.  Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema: “Hii Hija itakuwa ni urasimu tu na Msikiti Mtakatifu wa Makka umebadilishwa kuwa jumba la makumbusho ambapo watakaohiji ni wale tu walioidhinishwa na utawala wa Saudia. Hii si Hija ambayo Mwenyezi Mungu SWT ameitaja katika aya ya 27 ya Suratul Hajj ifuatavyo: Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.”

3928995

Kishikizo: saudia umrah waislamu
captcha