IQNA

Sheikh Shahat Anwar akisoma aya za Surah Al-Hadid (Video)

16:02 - October 13, 2020
Habari ID: 3473256
TEHRAN (IQNA) - Qarii maarufu wa Qur'ani Tukufu Sheikh Mahmoud Shahat Anwar hivi karibuni alisoma Qur'ani katika hafla ya kidini nchini humo.

Katika klipu hii ya hivi karibuni, Sheikh Shahat anasikika akisoma aya za 2 na 3 za Surah Al-Hadid zisemazo: " Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye uweza wa kila kitu. Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu."

Al-Hadidi ni Surah ya 57 ya Qur'ani Tukufu na ina aya 29. Al-Hadid maana yake ni chuma na neno hilo limetumika katika aya ya 25 ya Surah hiyo.

3928964

captcha