IQNA

Ammar Hakim: Iraq haitaanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni

12:43 - October 18, 2020
Habari ID: 3473271
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Mrengo wa Kitaifa wa al-Hikma wa Iraq amelaani vikali siasa za baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika eneo la Asia Magharibi za kufanya mapatano na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, nchi yake katu haitafanya mapatano na utawala huo ghasibu.

Ofisi ya Sayyid Ammar Hakim imetoa taarifa na kutangaza kuwa, Ammar Hakim ameashiria kadhia ya Palestina alipokutana na kufanya mazungumzo ofisi kwake na viongozi wa kaumu na shakhsia watajika  wa Iraq na kubainisha kwamba, haki ya Palestina haiwezi kupotea kwa kupita zama.

Kiongozi huyo wa Mrengo wa Kitaifa wa al-Hikma wa Iraq amesisitiza msimamo wake wa kupinga siasa za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kueleza kwamba, Iraq katu haiwezi kuwa sehemu ya siasa za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala vamizi wa Israel ambao unafanya mauaji kila leo dhidi ya Wapalestina sambamba na kupora ardhi zao.

Tarehe 15 Septemba mwaka huu, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain walitia saini makubaliano ya kutangaza uhusiano wa kawaida baina ya nchi zao na utawala ghasibu wa Israel.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Ikulu ya Marekani, White House, zilihudhuriwa pia na rais wa Marekani, Donald Trump na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala dhalimu wa Israel.

3929732

captcha