IQNA

Al-Azhar: Kufungamanisha Uislamu na ugaidi ni ishara ya ujinga

13:57 - October 20, 2020
Habari ID: 3473277
TEHRAN (IQNA) – Imamu Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amewakosoa vikali wale ambao wanajaribu kuufungamanisha Uislamu na ugaidi.

Katika ujumbe kupitia Twitter, Sheikh Ahmed el-Tayyib,  amesema: “Dhana kuwa Uislamu na uhusiano na ugaidi ni ishara ya ujinga. Dhana hii inaonyesha kutoheshimu itikadi za wengine na ni mfano ya kuchochea ghasia na kuumiza hisia za Waislamu zaidi ya bilioni moja duniani.”

Kauli hiyo ya Sheikh el Tayyib imekuja baad aya baadhi ya viongozi wa Ufaransa kutoa matamshi yenye chuki dhidi ya Uislamu baada ya mwalimu mmoja wa historia nchini humo kuuawa katika hujuma na mtu mwenye misimamo mikali ya kidini. Mwalimu huyo, Samuel Paty, alikatwa kichwa katika mtaa mmoja wa Paris  Ijumaa. Mwalimu huyo aliwakasirisha wengi baada ya kuonyesha katuni zinazomvunjia heshimua Mtume Muhammad SAW kwa wanafunzi wake.

Rais wa Ufarana Emmanuel Macron alitaja mauaji ya mwalimu huyo kuwa, ‘hujuma ya kigaidi ya Kiislamu’, huku akimtetea mwalimu huyo.

Macron pia hivi karibuni alikosolewa kwa kuutaja Uislamu kuwa dini ambayo iko katika mgogoro kote duniani.

3930284

captcha