IQNA

Misikiti kulindwa na polisi Ufaransa baada ya kupokea vitisho

14:09 - October 22, 2020
Habari ID: 3473284
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Ufaransa Gerarld Darmanin ameamuru polisi kulinda misikiti katika miji ya Bordeaux na Bexiers kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya misikiti kupokea vitisho vya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Katika ujumbe kupitia Twitter, amesema 'Vitisho kama hivyo havikubaliki katika ardhi ya Jamhuri,'.

Vitisho hivyo vimekuja baada ya mwalimu mmoja wa historia nchini humo kuuawa katika hujuma na mtu mwenye misimamo mikali ya kidini. Mwalimu huyo, Samuel Paty, alikatwa kichwa katika mtaa mmoja wa Paris  Ijumaa. Mwalimu huyo aliwakasirisha wengi baada ya kuonyesha katuni zinazomvunjia heshimua Mtume Muhammad SAW kwa wanafunzi wake.

Mwezi Septemba pia Jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo , lilichapisha vibonzo vinavyomkebehi na kumvunjia heshima Mtume wa mwisho wa Mwenyezi, Muhammad SAW. Aidha nchini Norway na Sweden wanasiasa wenye misimamo mikali wameshiriki katika vitendo vya kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Vitendo hivyo viovu vimelaaniwa na Waislamu, wasomi, maulama na wanasiasa katika nchi mbalimbali za duniani. 

3472901

Kishikizo: ufaransa misikiti
captcha