IQNA

Msweden aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad SAW aangamia katika ajali mbaya barabarani

19:41 - October 04, 2021
Habari ID: 3474382
TEHRAN (IQNA)- Mchora vibonzo mkaidi wa Sweden, Lars Vilks, ambaye amekuwa akilindwa na kupewa usalama na maafisa wa polisi wa nchi hiyo tokea mwaka 2007 baada ya kuchora vibonzo vya kumdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW), amekufa katika ajali mbaya ya barabarani.

Vilks (75) aliaga dunia jana Jumapili, baada ya gari lililokuwa limembeba akiwa pamoja na maafisa wawili wa polisi kugongana ana kwa ana na lori katika mji wa Markaryd, kaunti ya Kronoberg kusini mwa Sweden.

Carina Persson, mkuu wa polisi wa kaunti hiyo amethibitisha habari hiyo na kueleza kuwa, Vilks pamoja na askari polisi wawili waliokuwa wakimlinda wameangamia katika ajali hiyo ya jana.

Lars Vilks and the car crash that killed him.

Ameongeza kuwa, magari mawili yaliyohusika katika ajali hiyo ya jana yameteketea moto, lakini dereva wa lori amenusurika kifo, ingawaje amejeruhiwa vibaya.

Vilks ambaye alichora vibonzo vilivyomjunjia heshima Mtume SAW na kupelekea kuibuka maandamano kote duniani mwaka 2007, ameponea chupu chupu kuuawa mara kadhaa.

Moja ya katuni za kukirihisha alizochora raia huyo wa Denmark na kuwaghadhabisha mno Waislamu kote duniani, ni ile ya eti kichwa cha Mtume Mtukufu, kilichoungwa na mwili wa mbwa.

Nchi za Magharibi kwa miaka mingi sasa zimekuwa zikiunga mkono na hata kuyashajiisha majarida ya bara Ulaya kuchora vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu, Muhammad SAW.

3475904

captcha