IQNA

Waliohifadhi Qur’ani Al-ʾIskandariyah Misri waenziwa

20:11 - October 08, 2021
Habari ID: 3474398
TEHRAN (IQNA)- Watu 100 waliohifadhi Qur’ani Tukufu nchini Misri katika mji wa Al-ʾIskandariyah (Alexandria) wameenziwa na kutunukiwa zawadi baada ya mashindani makubwa ya Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa sherehe za kufunga mashindano makubwa ya Qur’ani Tukufu ya mkoa wa Al-ʾIskandariyah ambayo yamefanyika kwa himaya ya Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar zimefanyika jana Alhamisi na kuhudhuirwa na wakaazi wa maeneo ya An Nahdha na Al Amriya katika mji huo.

Katika sherehe hizo watu 100 waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu walienziwa na kutunukiwa zawadi.

Mkuu wa mkoa wa Al-ʾIskandariyah amehutubu katika sherehe hiyo na kusema mashindano hayo yanafanyika kwa mwaka wa kumi mtawalia  ambapo amewashukuru wazazi na waalumu kwa kufanya jitihada maradufu kuwafunza watoto Qur’ani Tukufu na kuwapa malezi bora.

 
 
تجلیل از 100 حافظ قرآن در اسکندریه مصر +عکس
 
تجلیل از 100 حافظ قرآن در اسکندریه مصر +عکس
 
تجلیل از 100 حافظ قرآن در اسکندریه مصر +عکس
 
تجلیل از 100 حافظ قرآن در اسکندریه مصر +عکس
 
تجلیل از 100 حافظ قرآن در اسکندریه مصر +عکس

 

4003170

captcha