IQNA

Kikao cha Kazakhstan chabaini

Chuki dhidi ya Uislamu ni kizuizi kikubwa katika kupatikana amani duniani

17:09 - October 09, 2021
Habari ID: 3474401
TEHRAN (IQNA)- Washiriki wa kikao kimoja cha kidini nchini Kazakhstan wametaja chuki dhidi ya Uislamu kuwa moja ya vizingiti vikubwa katika kufikiwa amani duniani.

Mkutano huo wa kikosi kazi cha Sekretarieti ya Viongozi Dini Duniani umefanyika katika mji mkuu wa Kazakhstan, Nur-Sultan.

Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na jumuia za kidini za Pakistan, Iran, Saudi Arabia, Uturuki, Misri, Jamhuri ya Azerbaijan, Russia, India, Uingereza na Vatican walishiriki katika kikao hicho.

Wazungumzaji katika kikao hicho wameipongeza Kazakhstan kwa kuandaa mkutano huo wa mazingumzo baina ya dini mbali mbali duniani.

Kati ya waliozungumza katika kikao hicho ni Allahshukur Hummat Pashazade ambaye ni Sheikh ul-Islam na Mufti Mkuu wa eneo la Kavkazia (Caucasus), Miguel Angel Moratinos, Mwakilishi Mkuu wa  Muungano wa Staarabu katika Umoja wa Mataifa, Zahra Rashidbeigi, Mkuu wa Kundi la Mazungumzo Baina ya Uislamu na Ukristo wa Kiothodoxi katika Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu.

Katika hotuba yake, Moratinos  amesisitiza kuhusu umuhimu wa dini katika jamii katika kuleta mazingira salama ya amani endelevu dunaini. Naye Sheikh Pashazadeh amesema chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia ni kizingiti katika kufikiwa amani dunaini. Ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wawakilishi wa dini mbali mbali kushirikiana katika kustawisha thamani bora katika jamii.

Kwa upande wake Bi Rashidbeigi amesisitiza kuhusu nafasi ya viongozi wa kidini katika kumaliza vita na mizozo duniani. Ametoa wito kwa wote kuahidi kuhimiza amani na watu kuishi pamoja kwa maelewano sambamba na kufanya jitihada za kuondoa fikra za kibaguzi na misimamo mikali kwa maslahi ya wanadamu wote.

4003304

captcha