IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Maadui wamekithirisha vita vya vyombo vya habari kuliko vita vya kiuchumi

17:08 - October 12, 2021
Habari ID: 3474416
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuwa vita vya vyombo vya habari vya maadui vimevizidi nguvu na kasi vita vya kiuchumi na kwamba hata maadui wa mapinduzi wananufaika na vita hivyo vya vyombo vya habari katika vita vyao vya kiuchumi dhidi ya mataifa mengine.

Muhammad Baqir Qalibaf amesema kuwa fikra za Imam Khomeini (M.A) na Mapinduzi ya Kiislamu katika miongo iliyopita zilikuwa na manufaa makubwa ambapo hivi sasa tumesimama imara mkabala wa adui mwenye nguvu. Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amebainisha hayo leo katika hafla ya kufunga duru ya pili ya uteuzi wa athari zilizofanya vizuri katika harakati ya muqawama na kulinda haram tukufu ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili.  

Qalibaf ameongeza kuwa suna ya Mwenyezi Mungu na wananchi wenye imani ni kigezo kile cha kujitetea kutakatifu cha walinzi wa haram ambacho kimepatikana katika eneo na kuweza kupigana vita na Daesh katika hali ambayo hakuna jeshi lolote lililoweza kukabiliana na kundi hilo la kigaidi.  

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa walinzi wa haram ni vikosi na askari ambao wanachama wake wametoka katika vijiji na miji mbalimbali katika Ulimwengu wa Kiislamu na kisha kujumuika pamoja chini ya maktaba ya Uislamu na Qurani Tukufu. 

4004367

captcha