IQNA

Wasomi Waislamu waslioshinda Tuzo ya Mustafa SAW 2021 watangazwa

20:39 - October 13, 2021
Habari ID: 3474418
TEHRAN (IQNA)- Mkurugenzi wa Taasisi ya Mustafa (saw) amesema kuwa wanasayansi watano Waislamu wametunukiwa tuzo ya taasisi hiyo ya mwanasayansi bora katika Ulimwengu wa Kiislamu mwaka huu wa 2021.

Mkuu wa Taasisi ya Mustafa, Mahdi Saffarinia amesema kuwa sherehe ya kukabidhi Tuzo ya Mustafa 2021 itafanyika rasmi tarehe 21 Oktoba katika Ukumbi wa Vahdat mjini Tehran na kwamba kazi za wanasayansi zitaonyeshwa kwenye sherehe hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Saffarinia amesema kuwa katika mchakato wa miaka miwili, kazi za wanasayansi Waislamu na watafiti zimechunguzwa ili kupata wanasayansi waliochaguliwa.

Ameongeza kuwa, Tuzo ya Mustafa inatolewa kwa wanasayansi ambao kazi zao za ubunifu zinawasilishwa kwa mara ya kwanza ulimwenguni.

Tuzo ya Mustafa hutolewa katika uwanja wa fizikia kwa wanasayansi bora wa Kiislamu ambao wanaishi na kufanya kazi ndani ya nchi za Waislamu na nje ya nchi hizo.

Washindi wa tuzo hiyo katika nyanja zote za Sayansi na Teknolojia ni msomi Muirani Profesa Cumrun Vafawa wa Chuo Kikuu cha Harvard kwa kazi yake "F-Theory" na Zahid Hasan kutokana na kazi yake ya "Weyl fermion semimetals." Zahid Hasan mwenye asili ya Bangladesh kwa sasa ni profesa katika Chuo Kikuu cha Princeton huko New Jersey nchini Marekani.

Washindi wa Tuzo ya al Mustafa 2021 kutoka ndani ya nchi za Kiislamu ni Yahya Tayalati kutoka Moroco, Prf. Mohamed H. Sayegh wa Lebanon na Muhammad Iqbal Choudhary wa Pakistan.

Tuzo ya Mustafa hutolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kila baada ya miaka miwili kwa wasomi na wanasayansi bora wa Ulimwengu wa Kiislamu waliovumbua mambo mbalimbali katika masuala ya  sayansi na teknolojia kwa ajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu.

Washindi wa Tuzo ya Mustafa SAW hupata zawadi ya nusu milioni dola pamoja na cheti.

Sherezi za kuwatangaza washindi wa Zawadi ya Mustafa SAW hufanyika katika Wiki ya Umoja wa Kiislamu nchini kama sehemu ya kuadhimisha Maulid ya Bwana Mtume Muhammad SAW.

84502085

captcha