IQNA

Hali ya Waislamu India

Al-Azhar yataka hatua za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu duniani

12:03 - June 16, 2022
Habari ID: 3475381
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Waislamu duniani.

Kikirejelea ukatili wa hivi majuzi dhidi ya Waislamu kuvunjiwa heshima Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) nchini India, kituo hicho kilitaja hatua hizo kuwa ni za kikatili na zisizo za kimaadili, kikisema zinakiuka mikataba ya haki za binadamu.

Aidha taarifa hiyo imesema kile ambacho kimekuwa kikifanyika nchini India ni kukejeli sheria zote zinazozingatia matusi kwa matakatifu ya kidini kama uhalifu.

Al-Azhar ilionya kwamba kuendelea kwa hatua hizo zisizo za kibinadamu dhidi ya Waislamu nchini India kutazidisha mivutano na kuzusha chuki na ubaguzi, jambo ambalo linaweza kusababisha vifo vya watu wasio na hatia.

Kituo hicho kilitoa wito kwa jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuchukua hatua ili kuzuia kujirudia kwa vitendo vinavyochochea hisia za Waislamu wa India.

Pia imetaka uchunguzi ufanyike kuhusu ubomoaji wa nyumba za Waislamu na mateso ya Waislamu nchini India na kudhaminiwa kukomeshwa kwa hatua za chuki dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Kusini mwa Asia.

Mapema wiki hii, Amnesty International iliitaka serikali ya India kukomesha mara moja ukandamizaji dhidi ya Waislamu ambao wamepinga matamshi ya matusi ya maafisa wa chama tawala BJP kuhusu Mtume Muhammad (SAW).

Waandamanaji wawili waliuawa na mamia ya wengine kukamatwa wiki iliyopita katika maandamano ya nchi nzima kuhusu matamshi yenye chuki, ambayo yaliiingiza India katika ghasia za kidiplomasia na kusababisha ghadhabu kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kanda za tingatinga zikibomoa nyumba za waliokamatwa au kutambuliwa kama waandamanaji zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mamlaka zilikuwa "zikiwasaka kwa ukali na kuwakandamiza Waislamu wanaothubutu kulalamikia ubaguzi unaowakabili," Aakar Patel wa Amnesty alisema katika taarifa yake Jumanne.

"Kukabiliana na waandamanaji kwa kutumia nguvu kupita kiasi, kuwekwa kizuizini kiholela na ubomoaji wa nyumba kama adhabu... ni ukiukaji kamili wa ahadi za India chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu."

Zaidi ya watu 300 wamekamatwa katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh kwa kujiunga na mikutano ya wiki iliyopita.

4064624

captcha