Video ya kamera ya usalama inamuonyesha mshukiwa wa kike, aliyetambuliwa kama Suzette Thompson mwenye umri wa miaka 57 wa Thief River Falls, akitumia kopo la kupulizia na kiberiti cha gesi kuteketeza pazia ndani ya jengo hilo kabla ya kuondoka haraka kwenye eneo la tukio.
CAIR tawi la Minnesota imesema inaunga mkono kuainisha tukio hilo kama uhalifu wa chuki, kufuatia kukamatwa kwa Thompson, ambaye alishtakiwa kwa makosa mawili ya uchomaji moto wa digrii ya kwanza.
"Sisi kama jumuiya tumepatwa na kiwewe," alisema mjumbe wa CAIR-MN Imam Mohammed, "Wanajamii wetu wana hofu."
Ripoti iliyotolewa na CAIR mwezi Aprili mwaka 2021 ilibaini kuwa Marekani kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 9 ya idadi ya malalamiko ya unyanyasaji dhidi ya Waislamu ambayo yalipokewa mwaka wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.
Kwa upande wake Baraza la Jumuiya za Kiislamu nchini Marekani limemwandikia barua Rais wa nchi hiyo, Joe Biden likisisitiza kuwa, kuwepo mwakilishi maalumu wa kusimamia na kupambana na chuki na propaganda chafu dhidi ya Uislamu kunaweza kusaidia juhudi za kupata suluhisho la tatizo hilo ambalo linaizonga jamii ya Waislamu nchini Marekani.
3479342