IQNA

Qur'ani Tukufu inasemaje/10

Namna shetani anavyomzuia mwanaadamu kufuata njia ya Mwenyezi Mungu

10:56 - June 23, 2022
Habari ID: 3475413
TEHRAN (IQNA) – Katika kufuatia njia ya mwongozo wa Mwenyezi Mungu kuna maadui na hivyo ili kukabiliana nao ni muhimu kwanza kutambua udhaifu wetu ili kuelewa njia ambazo maadui hawa hutumia kujipenyeza na kutuathiri.

Tangu Mwenyezi Mungu alipomuumba mwanadamu, shetani amekuwa akijaribu kuwapotosha wanadamu kutoka kwenye njia ya haki na kweli na kuwapotosha. Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaonya wanadamu juu ya uadui huu ndani ya Qur'ani Tukufu.

Lengo kuu la Shetani ni kumdanganya na kumhadaa mwanadamu ili asimtii Mwenyezi Mungu na kumfanya aelekee miungu ya uwongo. Wanadamu wako huru kabisa kuamua juu ya mwito wa Shetani na wakikubali kuhadaika, wanapaswa kulaumiwa.  "Na Shetani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu." (Surah Ibrahim, Aya ya 22)

Qur'ani imeleta njia kadhaa ambazo Shetani anazitumia kumuathiri mwanadamu: “Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehem" (Surah An-Nur, Aya ya 21)

Qur'ani Tukufu inabainisha namna ambavyo  Shetani anajaribu kuwahadaa watu hatua kwa hatua.

“…lakini Shetani aliwapambia vitendo vyao. Kwa hivyo leo yeye ndiye rafiki yao; nao watapata adhabu chungu." (Surah An-Nahl, Aya ya 63)

Mwandishi wa Tafsiri ya Qur'ani ya Nur Sheikh Muhsin Qaraati anarejelea nukta mbili katika aya hii:

- Moja ya njia za shetani ni kufanya dhambi na upotofu kuvutia kwa mwanadamu

- Kukubali mwaliko wa Shetani ni utangulizi wa utawala na mamlaka yake wake juu ya mwanadamu

Kupora motisha ya Mwanadamu ya kusonga mbele kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, kumfanya mtu amsahau Mwenyezi Mungu, kutoa ahadi za uongo na udanganyifu mwingine mwingi ni njia nyinginezo za shetani. Qur'ani Tukufu imemuonya mwanadamu dhidi yao.

Habari zinazohusiana
captcha