IQNA

Ugaidi barani Afrika

Indhari ya Al-Azhar kuhusu kuongezeka ugaidi nchini Mali

22:47 - June 26, 2022
Habari ID: 3475428
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Kupambana na Ugaidi ya Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri imetahadharisha kuhusu kuongezeka kwa vitendo vya magaidi nchini Mali.

Idara hiyo imesema kuongezeka kwa ugaidi nchini humo ni matokeo ya kuongezeka kwa idadi ya magaidi katikati na magharibi mwa Afrika, hasa nchini Burkina Faso.

Idara ya Kupambana na Ugaidi ya Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar ilisema kuwa shughuli za magaidi nchini Mali zimewalazimu maelfu ya watu kuondoka makwao na kukimbilia eneo karibu na mpaka na Niger.

Mali imekuwa ikipambana na makundi ya wanamgambo wanaofungamana na mitandao ya kigaiadi ya  al-Qaeda na Daesh (ISIL au ISIS) kwa takriban muongo mmoja, huku karibu theluthi mbili ya maeneo yake nje ya udhibiti wa serikali.

Magaidi hao wakufurishaji wanaofuata itikadi potovu ya Uwahhabi walianza operesheni nchini Mali mwaka 2012, na mzozo huo umeenea katika nchi jirani za Niger na Burkina Faso, na kuua na kuwakosesha makazi maelfu ya raia.

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni, idadi ya watu waliouawa katika robo ya kwanza ya 2022 na vikundi vya kigaidi na itikadi kali pamoja na vikosi vya usalama nchini Mali iliongezeka mara nne katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ya 2021, kutoka 128 hadi 543.

4066617

Kishikizo: mali ugaidi al azhar daesh
captcha