IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Serikali za Ulaya zinafadhili chuki dhidi ya Uislamu

21:14 - September 30, 2022
Habari ID: 3475859
TEHRAN (IQNA) – Mashirika ya kiraia ya Kiislamu yameshutumu nchi za Ulaya kwa kukandamiza jamii za Kiislamu, na hivyo kuzusha hali ya wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya Uislamu inayofadhiliwa na serikali barani Ulaya.

Ufaransa, Denmark na Austria zilikuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza sera ambazo wanaharakati walisema zinachangia "kukandamiza kimfumo jumuiya za kiraia za Kiislamu".

Akihutubia Kikao cha Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) huko Warsaw Alhamisi, Lamies Nassri, meneja wa mradi katika Kituo cha Haki za Waislamu (CEDA) nchini Denmark, alisema chuki dhidi ya  Uislamu inaenea kote Ulaya na kuzitaka serikali kulinda raia wao Waislamu.

Nassri aliwaambia wajumbe: "Ni jukumu lenu kama nchi wanachama kuhakikisha kwamba raia katika nchi hizi wanachama wanalindwa dhidi ya ubaguzi wa rangi, ufuatiliaji, unyanyapaa na mashambulizi. Akiangazia hali nchini Denmark, Nassri alisema chuki dhidi ya Uislamu ilikuwa "inawezeshwa moja kwa moja kupitia sera ya serikali " na "si suala la mrengo mkali wa kulia bali linashirikiwa katika wigo wa kisiasa".

Nassri alisema Waislamu wengi nchini Denmark walikabiliwa na ubaguzi kupitia kuainishwa kategoria ya wa watu kutoka asili zisizo za magharibi ambao, alisema, walionekana kama raia wa daraja la pili ikilinganishwa na Wadenmark asili.

Wanaharakati kutoka Ufaransa waliangazia athari kwa jumuiya za Kiislamu za kile kinachoitwa "hati ya maimamu" ambayo ilipitishwa mwaka jana na Baraza la Imani ya Kiislamu la Ufaransa kwa amri ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Elias d'Imzalene wa shirika lisilo la kiserikali la Kifaransa Perspectives Musulmanes alisema hati hiyo ni inalenga kulazimisha "Uislamu mpya kwa mujibu wa matakwa ya  serikali".

Mkutano huo pia ulisikia kutoka kwa Nehal Abdalla, ambaye alisemaPolisi wa Austria wa kukabiliana na ugaidi walivamia makao ya familia  70 za Kiislamu na kuwakamata wasomi na wanaharakati 30 katika operesheni ya Novemba 2020, lakini hakuna hata mmoja aliyeshtakiwa kwa kosa lolote.

3480675

captcha