IQNA

Maonyesho ya kwanza ya Qur’ani ya Senegal na Iran

19:20 - August 02, 2016
Habari ID: 3470487
Maonyesho ya kwanza na ya pamoja ya Qur’ani ya Iran na Senegal yamefanyika katika Msikiti wa Jamia wa Dakar, mji mkuu wa Senegal.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, taarifa ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO imesema kuwa, maonyesho hayo ya kwanza ya Qur’ani Tukufu na sanaa zinazohusiana na Qur’ani yamefanyika kwa ushirikiano wa Kitengo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran nchini Senegal ba Jumuiya ya Kitaifa ya Waalimu wa Qur’ani Senegal. Maonyesho hayo yaliyofanyika katika Msikiti wa Jamia wa Dakar, yalijumuisha picha na maandishi ya kaligrafia ya Qur’ani Tukufu na pia maudhui nyinginezo za kidini.

Maonyesho hayo yaliwavutia maafisa wa ngazi za juu wa kiutamaduni na umma kwa jumla hasa wanafunzi wa Qur’ani Tukufu.

Senegal ni nchi iliyo katika pwani ya Afrika Magharibi na asilimia 92 ya wakaazi wake ni Waislamu. Kwa mujibu wa nyaraka za historia, Uislamu ulifika Senegal katika karne ya 11 Miladia.


3519291
captcha