IQNA

Iran yaandaa kozi ya Qur’ani Tukufu nchini Senegal

12:21 - August 01, 2017
1
Habari ID: 3471097
TEHRAN (IQNA)-Kituo cha utamaduni cha Iran nchini Senegal kimeandaa duru ya pili ya kozi ya kusoma Qur’ani Tukufu kwa msingi wa Tajwid.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kozi hiyo itafanyika Agosti 2-4 katika mji wa Touba kati mwa Senegal.

Warsha hiyo ya Qur’ani Tukufu inafanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kitaifa ya Shule za Qur’ani Senegal na Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran, (ICRO).

Aidha kozi itasimamiwa na mtaalamu maarufu wa Tajwidi kutoka Iran Ustadh Majid Zakilou.

Mji wa Touba una idadi ya watu zaidi ya 550,000 na ni wa pili kwa ukubwa Senegal baada ya mji mkuu Dakar.

Senegal ni nchi ya Kiislamu iliyo Afrika Magharibi na inapakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea upande wa kusini mashariki, Guinea-Bissau upande wa kusini amgharibi huku ikiizunguka Senegal kwa pande tatu isipokuwa katika pwani.

3624130

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Ntagungira Rashidi
0
0
Bisjmillah Rahamani Rahimi

Kusimama kidete mbele ya haki, kujitenga na dhuluma na ufusadi pia ikhiraswi na kuwajari wanyonge wanaodhulumiwa ulimwenguni kote kamwe Mwenyezi Mungu hawezi kujitenga na Jamuhuri hii teule ambayo ni mfano wa utawala wa Al Kaimu bin Askari anaengojewa.

Hivyo hofu ya madhalimu inatokana na kwamba bilashaka wanajua harakati hizi za Jamuburi ya kiisilamu ni maandalizi na chanzo cha kuangushwa kwa dhuluma ulimwenguni kote; hivyo hofu ya madhalimu inasababishwa na kwamba dalili zote zinawabainishia kuwa mkono wa Mtawala mukuu wa ulimwengu, unakurubia kushika hatamu za uongozi wa kusimamia utawala wa Allah (st) hivyo mambo wanayoyafanya madhalimu ni sawa na kutapatapa mfamaji na mwenye kuweweseka mwenye kusubili kuvuta punzi ya mwisho.
captcha