IQNA

Iran yaandaa warsha ya Qur’ani nchini Senegal

11:53 - August 08, 2016
Habari ID: 3470506
Kituo cha utamaduni cha Iran nchini Senegal kimeandaa warsha kuhusu kusoma Qur’ani kwa tajwid katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo ya siku tatu imefanyika katika tawi la Senegal la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW.

Halikadhalika warsha hiyo imefanyika kwa ushirikino wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni ‘Udiplomasia wa Qur’ani’.

Wataalamu 23 wa Qur’ani kutoka mikoa 14 ya Senegal wameshiriki katika warsha hiyo.

Qarii bingwa wa Iran Majid Zakilu alikuwa mhadhiri na mtaalamu wa warsha hiyo ambapo alitoa mafunzo kuhusu sayansi ya tajwid.

Akizungumza wakati wa kufungwa warsha hiyo, mwambata wa utamaduni katika ubalozi wa Iran nchini Senegal, Sayyed Hassan Esmati akiwa pamoja na Sheikh Mustafa Lu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Shule za Qur’ani Senegal wamesisitiza kuhusu nafasi ya Qur’ani katika umoja wa Umma wa Waislamu. Aidha wamesisitiza utayarifu wao kuendeleleza warsha kama hiyo.

Senegal ni nchi iliyo katika pwani ya Afrika Magharibi na asilimia 92 ya wakaazi wake ni Waislamu. Kwa mujibu wa nyaraka za historia, Uislamu ulifika Senegal katika karne ya 11 Miladia.

3520800

captcha