IQNA

Uingereza inaunga mkono ugaidi

20:19 - October 03, 2014
Habari ID: 1456638
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amesema kuwa, wananchi wa Iran wanaunga mkono mazungumzo ya nyuklia kati ya serikali na kundi la 5+1 sanjari na kuchungwa mistari myekundu ya Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesisitiza kuwa, kuendelea kurutubishwa madini ya urani kwa kiwango kinachohitajika nchini, kuendelezwa utafiti wa nyuklia, kuendelezwa shughuli za vituo vya Fordo na Natanz vya kurutubisha urani na kuendelea shughuli za kinu cha  maji mazito cha Arak, ni miongoni mwa mambo yanayopaswa kuzingatiwa na timu ya  mazungumzo  ya nyuklia ya Iran kwenye mazungumzo yake na kundi la nchi sita za kundi la 5+1.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amekosoa vikali matamshi machafu yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kwenye kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kwamba, Cameron alitoa tuhuma za urongo dhidi ya Iran. Ayatullah Khatami amesema kuwa, faili la Uingereza kwa wananchi wa Iran ni jeusi na kusisitiza kuwa, Uingereza ni muungaji mkono mkubwa wa ugaidi na kwamba London imekuwa ikiuunga mkono utawala ghasibu wa Israel unaoua watoto wa Palestina tangu utawala huo bandia ulipoanza kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina. Ayatullah Khatami amesema kuwa, wananchi wa Iran hawakuhitajia wala hawana haja ya kuboresha uhusiano na Uingereza, bali serikali ya London ndiyo inayotaka kuimarisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameukosoa  muungano wa kimataifa wa kupambana eti na kundi la kigaidi la Daesh na kusisitiza kwamba, muungano huo ni kiini macho na una malengo ya kishetani; kwani nchi hizo zinazodai kupambana na ugaidi, ndizo zilikuwa mstari wa mbele katika kuanzisha makundi ya kigaidi. 1456594

AIR

Kishikizo: Uingereza, Iran, ugaidi
captcha