IQNA

Aliyehusika na hujuma msikitini Kuwait akiri kuwa ISIS (Daesh)

15:47 - August 06, 2015
Habari ID: 3339565
Mshtakiwa muhimu zaidi wa shambulio la kigaidi ndani ya msikiti mmoja nchini Kuwait amekiri kuwa ni mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Abdulrahman Sabah Aidan Saud, ambaye ni mmoja wa washtakiwa asiye na uraia alieleza mbele ya mahakama hapo jana wakati kesi ya washtakiwa hapo ilipoanza kusikilizwa kuwa kabla ya kutekeleza shambulio la kinyama ndani ya msikiti wa Imam Sadiq (AS) alikuwa ameshajiunga na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. Saud aidha alikiri mbele ya hakimu kuwa alikwenda kwenye kijiji kimoja kilichoko karibu na mpaka wa Saudi Arabia kwa ajili ya kutafuta mkanda wa mada za miripuko utakaotumika katika shambulio hilo ambalo kundi la Daesh lilikiri kuwa ndilo lililohusika. Abdulrahman Sabah Aidan Saud, ambaye ndiye aliyemchukua kwa gari hadi msikitini Fahd al Qaba’a, gaidi aliyetekeleza jinai hiyo, alitiwa nguvuni pamoja na mtuhumiwa mwengine siku mbili baada ya shambulio hilo la kigaidi lililofanywa ndani ya msikiti wa Imam Sadiq (AS). Shambulio la kigaidi la uripuaji bomu ndani ya msikiti huo lililofanywa tarehe 26 Juni mwaka huu lilisababisha watu 27 kuuawa shahidi na wengine 227 kujeruhiwa. Kesi ya washtakiwa 29 wa kesi hiyo ambao ni wanaume 22 na wanawake saba ilianza kusikilizwa na mahakama maalumu ya Kuwait Jumanne …/

captcha