IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Qarii Najmu Saqib wa Bangladesh +Video

TEHRAN (IQNA)- Najmu Saqib ni qarii ambaye usomaji wake wa Qur'ani Tukufu umepata umashuhiri katika nchi yake na maeneo mengine duniani.

Qarii huyo aidha ameweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu. Kwa mfano mwaka 2013 alipata zawadi ya Riyali za Kisaudi 80,000 kutoka kwa Imam wa Msikiti Mtakatifu wa Makka baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kimataifa ya qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Klipu hii ni ya qiraa yake ya aya za 51-57 za Sura Anbiya ambayo ni sura ya 21 katika Qur'ani Tukufu. 51.Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wake zamani, na tulikuwa tunamjua. 52. Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia kuyaabudu? 53. Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu. 54. kasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwa katika upotofu ulio dhaahiri. 55. Wakasema: Je! Umetujia kwa maneno ya kweli au wewe ni katika wachezao tu? 56. Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliye ziumba. Na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo. 57. Na Wallahi! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya mkisha geuka kwenda zenu. 

4003217

Kishikizo: bangladesh ، qurani tukufu