IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 63

Sifa na Tabia za Wanafiki Ilivyoelezwa katika Surah Al-Munafiqun

16:42 - February 26, 2023
Habari ID: 3476628
TEHRAN (IQNA)-Wakati watu wanaotafuta ukweli na watu watukufu wanapoonyesha njia sahihi kwa watu, kuna baadhi ambao wanahisi maslahi yao yanatishiwa. Inavyoonekana wanakubali mabadiliko na maendeleo yaliyoletwa lakini mioyoni mwao, wanatafuta kuunda upotovu kwenye njia.

Hii ni tabia ambayo Qur'ani Tukufu inaielezea kuwa ni ile ya Munafiqun (mnafiki), na Sura Al-Munafiqun inawahusu.

Al-Munafiqun ni jina la sura ya 63 ya Quran. Ina Aya 11 na iko katika Juzuu ya 28. Ni Madani na Sura ya 105 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Munafiqun ni wingi wa neno Munafiq, lenye maana ya mtu ambaye ni kafiri moyoni mwake lakini anadai kuwa ni muumini.

Sura inazungumzia sifa na tabia za wanafiki na uadui wao na Waislamu. Inamuamuru Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kuwa mwangalifu kuhusu hatari za mnafiki na inawataka waumini kutoa sadaka katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuepuka kuwa na nyuso mbili.

Sura hii inaonyesha sura ya kweli ya mnafiki na njama zao dhidi ya Waislamu, ikisema watanyimwa msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu. Pia inaorodhesha mambo kama vile mali, vyeo na watoto, ambavyo vinawapotosha watu kutoka kwenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu.

Suala la kumjua mnafiki limekuwa likitiliwa mkazo tangu ujio wa Uislamu kwa sababu matamshi na tabia zao zilizusha mizozo baina ya makundi mbalimbali ya Waislamu. Sura inataja sifa za mnafiki na inasisitiza kwamba Muslim ajiepushe nazo.

Dalili ya kwanza ya unafiki ni tofauti kati ya Zahir (kuonekana) na Batin (yaliyomo ndani ya mioyo yao). Wanasema kwa maneno kwamba wao ni waumini lakini hakuna imani mioyoni mwao. Ishara nyingine ni kutumia viapo ili kufikia malengo yao.

Muonekano wao wa kimwili unavutia na wanazungumza kwa kupendeza, hata hivyo, wao ni kama vitalu vya mbao katika nguo zenye mistari. Hawana uhuru na nia kali. Siku zote kuna hofu mioyoni mwao na daima wana mashaka na kutokuwa na uhakika.

captcha