IQNA

Mawaidha

Kigezo cha uzuri na wema mkabala wa kueneza chuki

19:09 - July 15, 2023
Habari ID: 3477287
TEHRAN (IQNA) – Kwa bahati mbaya, mchakato wa kufafanua dini kuiingiza katika jamii umechukua mwelekeo ambao wakati mwingi hisia za uzuri na wema wa mwanadamu umepuuzwa.

Haya ni kwa mujibu wa Ahmad Mobaleghi, mjumbe wa Baraza la Wanauoni Wataalamu la Iran, katika makala kwa IQNA. Hii hapa ni sehemu ya makala hiyo:

Wakati Qur'ani Tukufu inapomtambulisha Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) kama kigezo cha kuigwa, inalenga kumtambulisha kama kigezo cha maisha ya mwanadamu na jamii ya wanadamu na inapotumiwa maneno 'mfano mwema' ina maana kwamba Mungu anataka. kusema njia hii ya mfano wa kuigwa inapatana na uzuri (uzuri ambao asili ya mwanadamu inatafuta).

Kwa bahati mbaya, mchakato wa kubainisha dini kuiingiza katika jamii, umekuwa kiasi kwamba hisia za uzuri katika mwanadamu zimepuuzwa. Kiasi kwamba wakati mwingine baadhi hufikiri chochote chenye mapambano hakiendani na dini na chochote ambacho ndani yake kuna ukweli wa dini kiko mbali  na uzuri au umaridadi. Hii ni katika hali ambayo,  Qur'ani Tukufu inasema: “Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua..” (Aya 32 ya Surat Al-A’raf).

Mambo mawili yanaweza kupatikana kutokana na yale yaliyosemwa. Kwanza, dini haipuuzi hisia za mapambo katika dhati ya wanadamu kwani kwa hakika inatilia maanani urembo au mapambo. Pili, dini haiwaingizii Waislamu mfano wa kuigwa ambao uko mbali na urembo. Kinyume chake, sifa bora ya mfano huu ni uzuri, uzuri ambao ni katika asili ya mwanadamu.

Miongoni mwa matukio ya uzuri ambayo yako wazi katika tabia za Mtukufu Mtume (SAW) mtu anaweza kuashiria mwingiliano wake na jamii. Alitilia maanani sana kujenga wema katika nyoyo badala ya kueneza chuki, na alisisitiza sana kuhusu udugu wa Kiislamu badala ya tofauti za kijamii, na maadili ya kijamii badala ya vurugu na migongano, na umoja katika Ummah badala ya ukabila, na kutazama mauaji kuwa ni haramu  huku akihimiza kuendeleza amani na usalama badala ya kueneza hofu na woga, n.k.

Makundi mengi katika ulimwengu wa Kiislamu hayaakisi dini kwa namna nzuri katika mwenendo, tabia, na mtazamo wao na ndiyo maana yamezua matatizo, uchungu na vurugu katika maisha ya watu wengine ambayo husababisha watu kuondoka kwenye dini.

Kishikizo: MAWAIDHA
captcha