IQNA

Mawaidha

Jini ni Nani?

21:20 - January 06, 2024
Habari ID: 3478159
IQNA – Majini ni miongoni mwa viumbe vya Mwenyezi Mungu vilivyo tengenezwa kwa moto na hadhi ya viumbe hawa ni chini kuliko ya wanadamu.

Majini hayaonekani kwa macho ya mwanadamu. Lakini wao, kama wanadamu, wana Taklif (wajibu) na watafufuliwa Siku ya Kiyama.

Sababu ambaye imepelekea wanadamu kuwa bora kuliko majini ni kwamba Mwenyezi Mungu alimuamuru Iblis ambaye alikuwa ni jini kumsujudia Adam (AS).

Katika Qur'ani Tukufu, sifa kadhaa za majini zimetajwa, zikiwemo zifuatazo:

1- Ni kiumbe kilichotengenezwa kwa moto.

"...Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto." (Aya ya 15 ya Surah Ar-Rahman)

2- Baadhi yao ni Waumini na wengine ni makafiri.

 Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.." (Aya ya 11 ya Surah Al-Jinn)

3- Wana siku ya kiyama.

"Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.." (Aya ya 15 ya Surah Al-Jinn)

4- Walikuwa wana elimu ya ghaibu, lakini ikaondolewa kwao.

"Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!" (Aya 9 ya Surah Al-Jinn)

5- Waliwasiliana na baadhi ya watu na kwa ujuzi wao mdogo wa baadhi ya siri wakawapoteza.

"Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi." (Aya ya 6 ya Surah Al-Jinn)

6- Baadhi yao walikuwa na nguvu maalum:

“Akasema: Afriti (Jini mwenye nguvu sana), katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu.” ( Aya ya 39 ya Surah An-Naml)

7- Wana uwezo wa kufanya baadhi ya mambo kwa ajili ya wanadamu:

“Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyayushia chemchem ya shaba. Na katika majini walikuwako walio kuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anaye jitenga na amri yetu katika wao, tunamwonjesha adhabu ya Moto unao waka.  Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyo ondolewa mahala pake. Enyi watu wa Daudi! Fanyeni kazi kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru.” (Aya 12-13 za Surah Saba)

8- Waliumbwa katika ardhi kabla ya kuumbwa wanadamu

" Na majini tuliwaumba kabla (ya mwandamu) kwa moto wa upepo umoto.." (Aya ya 27 ya Surah Al-Hijr)

Kuna dhana nyingi  kuhusu Majini miongoni mwa watu ambazo si sahihi lakini kuwepo kwa Majini duniani kunakubalika kwa kuwa hakuna msingi wowote katika kudai kwamba ni viumbe tunavyoviona tu ndivyo vilivyopo.

Wanasayansi wanasema viumbe ambavyo wanadamu wanaweza kutambua kwa hisi zao tano ni sehemu ndogo ya viumbe vilivyopo. Hivi majuzi tu wanadamu wamegundua viumbe vidogo ambavyo hatuwezi kuviona. Kabla ya hapo, hakuna mtu ambaye angeamini kwamba mamilioni ya viumbe vidogo viko kwenye tone la maji au damu ambavyo havionekani.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kwamba kuna viumbe mbalimbali duniani ambavyo hatuwezi kuvitambua kwa hisia zetu.

Kwa upande mmoja, Qur'ani Tukufu inazungumza kuhusu Majini na kutaja baadhi ya sifa zao na hivyo hakuna sababu ya kimantiki ya kukataa kuwepo kwao.

3486691

Kishikizo: al jinn
captcha