IQNA – Ukiwa katika Mtaa wa Tran Hung Dao, Kata ya Cau Ong Lanh, jijini Ho Chi Minh, Vietnam, Msikiti wa Jamiul Islamiyah unajitokeza kwa fahari katikati ya jiji hilo kwa usanifu wake unaofanana na ngome na rangi zake za kipekee za kijani.
Habari ID: 3482666 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/23
IQNA – Kutokana na changamoto za hali ya hewa nchini Singapore, vipindi vya hotuba za Swala ya Ijumaa vitafupishwa kwa muda kuanzia wiki hii.
Habari ID: 3482659 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/22
IQNA – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limetangaza kuwa Waislamu 255 wamechaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali za umma katika majimbo 26 ya Marekani mwaka 2026, idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa. Viongozi hao wanahudumu katika karibu kila ngazi ya serikali, wakiwemo wajumbe wa Kongresi, maseneta na wawakilishi wa majimbo, majaji, meya, wajumbe wa mabaraza ya miji, bodi za shule na nafasi nyingine za mitaa.
Habari ID: 3482656 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/21
IQNA – Kiongozi wa Kikristo katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria amemuenzo mwanazuoni wa Kiislamu, Sheikh Usman Mohammed Mai-Mota (Gwalli), kwa kutambua mchango wake wa zaidi ya nusu karne katika kutoa elimu ya Kiislamu na kuwafundisha maelfu ya vijana, katika juhudi za kuimarisha kuishi kwa amani na mshikamano kati ya Wakristo na Waislamu.
Habari ID: 3482651 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/20
IQNA – Misikiti ya kihistoria nchini Kosovo inapaswa kutazamwa kama sehemu ya msingi ya urithi wa kiutamaduni na kihistoria wa taifa hilo, si kama maeneo ya ibada pekee, afisa mmoja wa Jumuiya ya Kiislamu amesema.
Habari ID: 3482648 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/19
IQNA – Paul Pogba, nyota wa soka wa Ufaransa, ameonyesha mshikamano na Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, wanaokabiliwa na mauaj ya kimbari ya Israel, kwa kuposti picha ya mtoto wa Kipalestina akiwa miongoni mwa vifusi na uharibifu wa Gaza kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Habari ID: 3482645 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/18
IQNA – Mtandao wa Mazungumzo ya Kiislamu nchini Norway ulishiriki katika “Arendalsuka,” ambayo ni jukwaa la kila mwaka la mijadala ya umma nchini Norway. Katika jukwaa hilo, mtandao huo ulijadili masuala muhimu ikiwemo utambulisho wa kidini, uhuru wa kujieleza, ubaguzi, na tofauti iliyopo kati ya ukosoaji halali wa dini na chuki zinazolenga jamii nzima.
Habari ID: 3482632 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/16
IQNA – Katikati ya ukame usio wa kawaida na uhaba mkali wa maji unaotishia sekta ya kilimo na mazingira, wanazuoni wa Kiislamu nchini Uingereza wametoa wito kwa maimamu wa misikiti na waumini kufufua sunna tukufu ya “Istisqa” (Swala ya kuomba mvua).
Habari ID: 3482630 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/16
IQNA – Msikiti wa Minto (Masjidur Rahman Al-Jami’ee) uliopo New South Wales, Australia, imeandaa hafla maalum ya “Siku ya Wazi” siku ya Jumamosi, Agosti 15. Msikiti huu utafungua milango yake kwa jamii pana kwa ajili ya siku maalum iliyolenga huduma ya vijana, majadiliano ya dini tofauti, na kuimarisha maelewano katika jamii.
Habari ID: 3482625 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/15
IQNA – Katikati ya hofu inayokua kuhusu wimbi la chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) nchini Ujerumani, mamlaka zimeandikisha visa 231 vya uhalifu dhidi ya Waislamu nchini humo katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026.
Habari ID: 3482617 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/12
IQNA – Makumbusho yaliyojitolea kuhifadhi historia na utamaduni wa Waislamu wa Kitatar yanatarajiwa kuzinduliwa nchini Poland.
Habari ID: 3482612 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/11
IQNA – Kupokea vijana Waislamu na kuwapatia programu za kidini na Qur’ani huifanya misikiti nchini Brazil kuimarisha hali yao ya kiroho, huku pia ikilea kizazi kipya kilichounganishwa na Qur’an na Sunna ya Mtume SAW.
Habari ID: 3482606 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/09
IQNA – Vyombo vya habari vya Israel vimeonyesha wasiwasi kufuatia ushindi wa daktari Mmisri-Mmarekani, Abdul El-Sayed, katika kura za mchujo za Chama cha Democratic kwa kiti cha Seneti ya Marekani katika jimbo la Michigan, vikilitaja tukio hilo kuwa pigo muhimu kwa makundi yanayounga mkono Israel nchini Marekani.
Habari ID: 3482593 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/07
IQNA – Baraza la Jiji la McKinney, jimboni Texas nchini Marekani, limeidhinisha kwa kauli moja mpango wa kujengwa kwa msikiti mpya uliopendekezwa na Jumuiya ya Kiislamu ya McKinney, licha ya wasiwasi uliotolewa na baadhi ya wakazi kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kwa jamii inayozunguka eneo hilo. Uamuzi huo wa kura 7-0 ulifuatia kikao kirefu na wakati mwingine chenye mvutano, ambapo takriban wakazi 150 walizungumza, baadhi wakiunga mkono na wengine wakipinga mradi huo.
Habari ID: 3482592 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/07
IQNA - Tamasha la Salam 2026 limefanyika nchini Kosovo kwa ushiriki wa familia za Kiislamu, sambamba na uwasilishaji wa programu za kitamaduni na kisanii.
Habari ID: 3482546 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/28
IQNA – Taasisi ya British Muslim Trust (BMT) imebainisha kuwa, kwa wastani, msikiti mmoja hushambuliwa kila baada ya siku tano nchini Uingereza.
Habari ID: 3482532 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/25
IQNA – Mfanyakazi mmoja Mwislamu wa vibanda vya biashara amechomwa kisu zaidi ya mara 15 ndani ya kituo cha ununuzi (mall) huko Utah, Marekani, na mtu ambaye baadaye alikiri kwa polisi kuwa alikusudia kumuua “kwa sababu ya dini yake.”
Habari ID: 3482498 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/17
IQNA – Mamlaka za Uingereza zimemfungulia mashtaka kijana mmoja kufuatia uchunguzi wa njama zilizodaiwa kuwa zililenga kushambulia misikiti katika jiji la London.
Habari ID: 3482495 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/17
IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Vienna, jijini Vienna nchini Austria, kimekaribisha makundi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini humo siku kadhaa kabla ya kuanza kwa likizo ya masomo.
Habari ID: 3482479 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/13
iQNA – Kundi la wanawake Waislamu katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Kenya limefanikiwa kugeuza ari ya kujitolea kuwa mradi wa maendeleo unaochanganya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, huduma kwa Qur’an Tukufu, na kuimarisha mshikamano wa kijamii.
Habari ID: 3482426 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/01