IQNA – Harakati ya Muqawama wa Palestina ya Hamas imepongeza kauli ya Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, kuhusu umuhimu wa kusitishwa kwa vita katika ukanda wa Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
Habari ID: 3482623 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/14
IQNA – Katika tukio la kusikitisha na la kihistoria, miili ya mashahidi 112 imezikwa katika mazishi makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kushuhudiwa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3482590 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/05
IQNA-Katika mwendelezo wa kuonyesha ustahimilivu na ari ya kiimani katikati ya mapambano, wanafunzi 110 wa kike wenye kuhifadhi Qur’ani huko Gaza wamefanikiwa kuhitimisha usomaji wa Qur’ani nzima katika kikao kimoja cha Khatm al-Qur’an.
Habari ID: 3482585 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/04
QNA – Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imekaribisha kupitishwa kwa sheria nchini Ireland inayopiga marufuku uingizaji wa bidhaa kutoka vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Wizara hiyo imetoa wito kwa mataifa na mabunge yote duniani kuchukua hatua kama hiyo dhidi ya utawala unaokalia ardhi kwa mabavu.
Habari ID: 3482549 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/28
Mtazamo
IQNA – Mchambuzi wa kisiasa kutoka Lebanon anaamini kuwa mvutano unaoendelea katika Lango Bahari La Hormuz si mapambano ya kawaida juu ya njia ya majini, bali ni vita vikali vya kuamua hatima na utambulisho wa mfumo wa kiusalama katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3482543 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/27
IQNA – Kuongezeka kwa operesheni za muqawama au mapambano ya ukombozi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel kunaakisi kushindwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwazuia Wapalestina kusimama kutetea ardhi yao, haki zao, na maeneo yao matukufu.
Habari ID: 3482537 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/26
IQNA – Hafla maalumu imeandaliwa kwa ajili ya kuwatunuku zawadi na kuwaenzi vijana 600 waliohifadhi Qur’ani Tukufu katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3482530 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/24
IQNA – Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, imelaani uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem), ikionya kuwa vitendo hivi vya wazi vya uchokozi vitamalizika kwa hasara ya utawala ghasibu wa Israel na walowezi wa Kizayuni.
Habari ID: 3482529 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/24
IQNA – Magenge ya walowezi wa Kizayuni yamefanya mfululizo wa mashambulizi ya kikatili usiku wa Jumapili katika miji na vijiji mbalimbali katika wilaya za al-Khalil (Hebron) na Nablus katika eneo linalokaliw akwa mabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi, ambapo wamechoma moto nyumba na msikiti, wamewashambulia wakazi, na kupora mifugo huku wakilindwa na wanajeshi wa utawala katili wa Israel.
Habari ID: 3482514 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/20
IQNA-Afisa mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Palestina, Hamas, ametoa pongezi za dhati kwa Uhispania kufuatia ushindi wake baada ya mechi ngumu katika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2026, akielezea mafanikio hayo kuwa ni chanzo cha furaha kwa watu wa Palestina na wafuasi wote wa haki, huku akibainisha kuwa ushindi huo ni pigo hasa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na wafadhili wake.
Habari ID: 3482512 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/20
IQNA – Meya wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, amesema Jumamosi kuwa utawala wake unachunguza iwapo una mamlaka ya kisheria ya kumkamata Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, iwapo atatembelea jiji hilo kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba.
Habari ID: 3482506 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19
IQNA – Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ardhi za Palestina Zinazokaliwa kwa Mabavu, Francesca Albanese, ametoa wito siku ya Jumapili kwa hati ya haraka ya kukamatwa kwa Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni, Yisrael Katz, baada ya waziri huyo kukiri kufanya jinai za kivita huko Gaza na Lebanon.
Habari ID: 3482478 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/13
IQNA-Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (Hamas) iimelaani vikali uamuzi wa awali wa bunge la utawala wa Israel (Knesset) kupitisha muswada wa mrengo wa kulia wenye nia ya kupiga marufuku wito wa Sala ya Kiislamu (Adhana) kupitia vipaza sauti katika misikiti ya Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) na maeneo mengine yote yaliyovamia na kukaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3482428 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/02
IQNA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Mkataba wa Maelewano (MoU) wa kumaliza vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran haukuwa matokeo ya shinikizo au kulazimishwa, bali ni zao la ustahimilivu na nguvu ya taifa shupavu la Iran.
Habari ID: 3482399 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA – Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni umefeli katika njama zake zote za kutaka kuangamiza harakati hiyo ya mapambano (Muqawama).
Habari ID: 3482382 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/20
IQNA – Akieleza sababu za kukataa uhamisho wa mchezaji kwenda klabu ya soka ya Israel ya Maccabi Tel Aviv, mmiliki wa klabu ya soka ya Poland ya Pogon Szczecin ametolea mfano wa Ujerumani ya enzi za utawala wa Nazi.
Habari ID: 3482329 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/06
IQNA – Eneo takatifu na muhimu kwa Waislamu katika mji mtukufu wa al‑Quds (Jerusalem) litaanza kusimamiwa na maafisa wa polisi wenye misimamo mikali wa Kiyahudi wa mrengo wa kulia.
Habari ID: 3482325 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/05
IQNA-Umoja wa Mataifa umekosoa vikali mipango ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ya kupanua udhibiti juu ya Ukanda wa Gaza, na kusisitiza kuwa eneo lote ni haki ya watu wa Palestina.
Habari ID: 3482299 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/30
IQNA – Umoja wa Mataifa umelaani jinsi Israel ilivyowatendea wanaharakati waliokuwa katika meli za misaada zilizoelekea Gaza baada ya msafara huo kukamatwa katika maji ya kimataifa.
Habari ID: 3482270 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/22
IQNA – Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) imekataa rasmi mpango wa eneo linalojitenga la Somalia linalojulikana kama Somaliland w kufungua ubalozi katika mji wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
Habari ID: 3482269 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/22