IQNA

Serikali ya Nigeria yafikishwa ICC kufuatia mauaji ya Waislamu wa Kishia Zaria

17:52 - March 23, 2016
Habari ID: 3470211
Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza imetangaza kuwa faili la mauaji ya Waislamu katika mji wa Zaria nchini Nigeria limewasilishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague nchini Uholanzi.

Taarifa iliyotolewa na Kamisheni ya Haki za Binamu ya Kiislamu ya Uingereza (IHRC) imesema faili la mashambulizi na mauaji yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wa mji wa Zaria limepelekwa Hague katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, uhalifu uliofanywa na jeshi la Nigeria katika kipindi cha tarehe 12 hadi 14 Disemba katika mji wa Zaria dhidi ya Waisalmu ni jinai dhidi ya binadamu na kuna udharura wa kutolewa amri ya uchunguzi wa mahakama ya ICC kuhusu uhalifu huo.

IHRC imesisitiza kuwa ushahidi uliopo unathibitisha kwamba mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky yalikuwa yamepangwa.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Haki za Binamu ya Kiislamu ya Uingereza (IHRC) Bwana Mas'ud Shajareh amesema kuwa ukubwa wa jinai hiyo na mwenendo wa serikali ya Nigeria wa kupuuza mauaji hayo vinalazimu kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya mamia ya Waislamu katika mji wa Zaria.

Zaidi ya Waislamu elfu moja waliuawa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa dhidi ya kituo cha kidini cha Husseiniya  Baqiyatullah na nyumba ya kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria katika mji wa Zaria, Sheikh Ibrahim Zakzaky. Hadi sasa Sheikh Zakzakay na mke wake wangali wanashikiliwa   katika korokoro zakuogofya za Jeshi la Nigeria.

3484401

captcha