Mashindano hayo ya Qur'ani ya siku tano yanajumuisha wanafunzi 500 kutoka vyuo vikuu 21 vya umma katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo ya Qur'ani yana kategmoria nne ambao ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 20,10 na 5 kwa kuzingatia misingi ya tajwidi.
Waandalizi wametangaza kuwa washindi watatnukiwa zawadi kadhaa zikiwemo fedha taslimu.
Kwa mujibu wa Salahuddin Bauthman, mmoja kati ya wakuu wa kamati andalizi anasema mashindano hayo yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Jeddah ni mashindano makubwa zaidi ya Qur'ani kwa wanachuo nchini Saudi Arabia.