IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Vitendo vya kusikitisha vya kuvunjia heshima Qur'ani vyaendelea Uswidi

9:37 - April 28, 2024
Habari ID: 3478747
IQNA - Inaonekana hakuna nia nchini Uswidi ya kukomesha vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, vitendo ambavyo vimewasikitisha na kuwakasirisha Waislamu kote ulimwenguni.  

Siku ya Ijumaa, mwanamke wa Uswidi aliyekuwa amebeba msalaba alichoma nakala ya Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Skandinavia.

Kitendo hicho cha kufuru kilifanyika katika eneo la Skarholmen katika vitongoji vya mji mkuu, Stockholm, eneo ambalo hapo awali lilishuhudia vitendo kama hivyo vya kuvujia heshima Qur'ani Tukufu.

Mwanamke huyo alisema yeye ni Mkristo ambaye anaamini mafundisho ya Biblia na Ukristo lazima yatekelezwe nchini Uswidi.

Uislamu, misikiti na kila kitu kinachohusishwa na dini hiyo havina nafasi nchini Uswidi, aliongeza.

Baadaye mchana, makumi ya watu walifanya maandamano huko Stockholm, wakiimba nyimbo za kupinga ubaguzi wa rangi na kuvunjiwa heshima matakatifu ya kidini.

Mapema mwezi huu, Waislamu nchini Uswidi walipokuwa wakisherehekea Eid al-Fitr, nakala ya Qur'ani Tukufu ilivunjiwa heshima katika mji mkuu.

Uswidi imekuwa kitovu cha vitendo vya kuvunjia heshima nakala za Qur'ani.

Matukio hayo ya kuvunjiwa heshima Qur'ani yamezidisha mvutano kati ya nchi za Kiislamu zilizotaka kuchukuliwa vitendo viovu vya vya chuki dhidi ya Uislamu.

4212494

Habari zinazohusiana
captcha