IQNA

Utawala wa Kizayuni wamzuia afisa wa wakfu Palestina kuingia Al Aqsa

10:55 - November 05, 2020
Habari ID: 3473330
TEHRAN (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel umempiga marufuku naibu mkurugenzi wa Idara ya Wakfu ya Mji wa Quds (Jerusalem) kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa kwa muda wa miezi sita.

"Nilipokea taarifa ya Israel kuwa nimepigwa marufuku kuingia Al Aqsa kwa muda wa miezi sita," amesema Sheikh Najeh Bakirat. Amesema wakuu wa utawala wa Kizayuni hawakumpa sababu ya hatua yao hiyo. Aidha amesema maafisa wa kijasusi wa Israel waliihujumu ofisi yake wiki iliyopita wakidai yeye ni 'tishio kwa usalama wa Israel.'

Israel imempiga marufuku Sheikh Bakirat kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa mara 23 tokea mwaka 2001 ambapo pia amewekwa kizuizini mara 13. Amesema kitendo hicho ni njama ya Israel ya kuhakikisha idadi ya waumini inapungua katika Msikiti wa Al Aqsa sambamba na kuvuruga kati ya Idara ya Wakfu mjini Quds.

Msikiti wa Al Aqsa ni wa tatu kwa utakatifu kwa Waislamu. Mayahudi wanadai eneo hilo Al Asa ni milki yao na kwamba eti kuna mahekalu mawili ya Mayahudi.

Utawala wa Kizayuni ulikalia kwa mabavu eneo la mashariki la mji wa Quds, uliko msikiti wa Al Aqsa, mwaka 1967, hatua ambayo haitambuliwa na jamii ya kimataifa.

3473030

captcha