IQNA

Hamas: Netanyahu ameshindwa vibaya katika vita vya Ghaza

11:54 - May 20, 2021
Habari ID: 3473928
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) imetangaza ushindi katika mapambano ya siku 10 dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umevamia Ukanda wa Ghaza na kuongeza kwamba waziri mkuu wa utawala huo Benjamni Netanyahu ameshindwa vibaya katika makabiliano hayo.

Tokea Jumatatu 10 Mei, utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza mfululizo wa mashambulizi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza eneo ambalo ni makao makuu ya harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Jihad Islami. Harakati hizo mbili zimejibu hujuma ya Israel kwa kuvurumisha maelfu ya maroketi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina la Israel.

Akiungumza na Televisheni ya Al Mayadeen Jumatano, naibu kiongozi wa Hamas Mousa Abu Marzouq amesema Hamas imepata ushindi na Netanyahu ameshindwa vibaya. Aidha amesema :"Nataraji tutafikia mapatano ya usitishwaji vita wa muda katika kipindi cha siku moja au mbili zijazo."

Abu Marzouq amesema jibu kali la harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu kwa hujuma ya Israel ndio sababu ambayo imeilazimu Marekani iutake utawala wa Tel Aviv upunguza hujuma zake.

Jumatano Rais Joe Biden wa Marekani alimtaka Netanyahu achukue hatua za kusitisha mapigano katika Ukanda wa Ghaza. Abu Marzouq amesema Biden ametoa tamko hilo katika hali ambayo siku zilizopita Marekani ilizuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa taarifa ya kutaka Israel isitishe vita.

Kwa mujibu wa Ofir Gendelman, msemaji wa ofisi ya Netanyahu, makundi ya muqawama huko Ghaza yamevurumisha marokei 4,000 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu katika kujibu hujuma za Israel. Abu Marzouq amesema unyama wa Israel umepelekea Wapalestina wapata uungaji mkono kote duniani.

Tangu tarehe 10 mwezi huu wa Mei jeshi la utawala haramu wa Israel lilianzisha mashambulizi ya kikatili dhidi ya watu wa Palestina na hadi sasa Wapalestina zaidi ya 227 wameuawa shahidi, wakiwemo watoto 64 na wanawake 38, huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa.   

3474774

Kishikizo: ghaza hamas netanyahu vita
captcha