Mkuu wa Ofisi ya Mahusiano ya Umma ya Hizbullah Mohammad Afif amesema kitendo hicho kiovu cha Marekani kinalenga kuficha ukweli kuhusu jinai ambazo imezitenda pamoja na waitifakki wake dhidi watu wanaodhulumiwa katika eneo hasa watu wa Yemen na Palestina ambao wanakabiliwa na mzingiro mbaya zaidi.
Naye Qais Khazali, kiongozi wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya Iraq amelaani hatua ya Marekani kufunga tovuti za habari za Iran na harakati za muqawama katika eneo. Amesema kitendo hicho kinaweza wazi ukweli kuwa nchi za Magharibi zinahadaa zinapodai kutetea haki za binadamu na uhuru wa maoni. Amesema Marekani imeteka tovuti za habari ambazo zimekuwa zikipinga njama za Marekani, Uingereza, utawala wa Israel, Saudia na Imarati. Amesema kitendo hicho cha Marekani ni ithbati tosha kuwa imeshindw akijeshi na sasa imeamua kukpambana na fikra.
Juzi serikali mpya ya Marekani iliendeleza sera za kiijuba ya kibeberu za nchi hiyo kwa kuzifunga tovuti za televisheni za kimataifa za Iran na vyombo vya habari vya mrengo wa muqawama au mapambano ya Kiislamu Yemen, Palestina, Iraq na Bahrain.
Televisheni ya Kiingereza ya Iran ya Press TV na zile za Kiarabu za Al Alam na Al Khauthar ni kati ya vyombo vya habari ambavyo vimefunguiwa tovuti zao na Marekani.
Kufuatia hatua hiyo Press TV imetangaza kuwa tovuti iliyofungwa ya presstv.com sasa inapatikana kupitia presstv.ir