IQNA

Kumbukumbu ya kuasisiwa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina

17:22 - October 09, 2021
Habari ID: 3474402
TEHRAN (IQNA) Harakati ya Jihad Islami ya kupigania ukombozi wa Palestina imefanya maadhimisho kwa mnasaba wa kutumia mwaka wa 34 tangu kuasisiwa kwake.

Harakati hii iliyoundwa 6 mwezi Oktoba 1987ni kati ya harakati kongwe zaidi za mapambano  ya ukombozi huko Palestina. Harakati hiyo imekuwa na makatibu wakuu watatu katika kipindi cha miaka 34 iliyopita hadi hivi sasa. Shahidi Fathi Shiqaqi ni kiongozi wa kwanza na Katibu Mkuu wa Jihadul Islami ambaye aliuawa kigaidi na Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) mwaka 1995 katika mji wa Sliema katika kisiwa cha Malta wakati alipokuwa akirejea Palestina kutokea Libya.   

Dakta Ramadhan Abdalah Shallah alichukua hatamu za Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina baada ya kuuliwa shahidi Fathi Shiqaqi; hadi mwaka 2018. Mwaka huo Dakta Ramadhan Abdallah Shallah alipatwa na hali ya kutojitambua kwa kupoteza fahamu kutokana na kuugua maradhi na kupatwa na kiharusi na kisha kuuaga dunia Juni 6 mwaka 2020. Ziad al Nakhalah Katibu Mkuu wa sasa ni Katibu Mkuu wa tatu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ambaye amekuwa katika nafasi hiyo tangu Septemba 27 mwaka 2018 hadi sasa. 

Uadui wa utawala wa Kizayuni na Marekani

Nukta muhimu kuhusu viongozi wa Jihad Islami ya Palestina ni kwamba wote wamewekwa katika orodha ya kuuawa ya adui Mzayuni. Ziad al Nakhalah pia yuko katika faharasa hiyo ya kuuawa ya utawala wa Kizayuni. Mbali na hilo, Harakati ya Jihad Islami imetajwa na Marekani kama taasisi ya kigaidi. Marekani mwaka 1997 iliiweka Jihad Islami katika orodha ya makundi ya kigaidi yanayosakwa na nchi hiyo. Hatua kama hizi za utawala wa Kizayuni za kuwaua viongozi na makamanda wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina na pia hatua ya serikali ya Marekani ya kuwataja shakhsia hao kuwa ni magaidi zinatokana na imani na utendaji wa harakati hiyo ya Palestina katika kukabiliana na utawala huo ghasibu unaoikalia Quds kwa mabavu na kuimarisha mhimili wa muqawama.  

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina haiamini sana shughuli za kisiasa katika mazingira ya sasa ya Palestina. Ndio maana ikasusiai uchaguzi wa bunge wa mwaka 2006 huko Palestina; uchaguzi ambao Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) iliibuka na ushindi. Hata hivyo haukuzuia kuendelea vita vya ndani huko Palestina na hivyo kuifanya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuchukua madaraka, na tangu wakati huo hadi sasa hakujafanyika uchaguzi mwingine huko Palestina. 

Kipaumbele kwa muqawama 

Harakati ya Jihad Islami inatoa kipaumbele kwa muqawama katika siasa na harakati zake. Kwa msingi huo,  nguzo muhimu ya harakati hiyo ni tawi lake la kijeshi kwa jina la Saraya al Quds au brigedi za Quds. Makamanda wa Saraya al Quds siku zote wamekuwa wakiwekwa katika orodha ya viongozi wa muqawama wanaosakwa kuuliwa na Marekani na utawala ghasibu wa Kizayuni.  

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina kamwe haijachukua hatua za kufikia mapatano na kufanya mazungumzo na utawala wa Israel; na mazungumzo baina ya nchi za Kiarabu na Israel pia hayaathiri kivyovyote irada na azma ya harakati hiyo kwa ajili ya kukabiliana na utawalal huo. Ziad al Nakhalah Katibu Mkuu wa Jihad Islami ya Palestina amesisitiza katika hotuba yake kwa mnasaba wa maadhimisho ya kutimia mwaka wa 34 tangu kuasisiwa harakati hiyo kwamba, vita vya Saif al Quds vimewabainishia wazi walimwengu udhaifu na kushindwa utawala huo ghasibu na  wakati huo huo kuidhihirishia pakubwa dunia kuwa, hafla  za kuhuisha uhusiano, za kusherehekea amani ya uwongo na kuzindua balozi za utawala wa Kizayuni katika miji mikuu ya nchi za Kiarabu abadan haziziwezi kubadili uhakika wa kihistoria.  

Matunda ya harakati

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina si tu haijaachana na muqawama bali imeimarisha azma yake ya muqawama ili kukabiliana vilivyo na utawala wa Israel unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu. Oparesheni ya kutoroka jela iliyotekelezwa na mateka 6 wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali la Gilboa  ni miongoni mwa hatua za aina yake za kimuqawama. Watu watano waliotoroka katika gereza hilo la Israel walikuwa wanachama wa Jihad Islami ya Palestina. Kuhusiana na suala hilo, Talal Naji Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina anasema, oparesheni iliyojiri katika jela ya al Gilboa ni moja ya matunda ya harakati ya Jihad Islami. 

3240763

captcha