IQNA

Ujerumani yachapisha kitabu cha kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

14:06 - November 04, 2021
Habari ID: 3474515
TEHRAN (IQNA) – Kitabu chenye anuani ya "Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia): Kabiliana Nayo kwa Jina la Amani" kimechapishwa kwa lugha ya Kiingereza nchini Ujerumani kwa ajili ya watoto.

Kitabu hicho kinatazamiwa kutoa mafunzo sahihi kwa watoto kuhusu Uislamu na namna ya kuishi na Waislamu kwa amani.

Hivi sasa mijadala kuhusu itikadi za kidini, hasa kuhusu Uislamu, ni maudhi muhimu katika nchi za Ulaya. Kumekuwa kukienezwa propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na watoto wameathirika vibaya na propaganda hizo.

Makundi ya kibaguzi  ya mrengo wa kulia barani Ulaya yamekuwa yakijaribu kutumia kila mbinu kuchafua fikra za watoto kuhusu Uislamu na kwa msingi huo baadhi ya nchi zimeanzisha mikakati ya kukabiliana na hali hiyo.

Maelezo kuhusu kitabu hicho katika tovuti ya Amazon yanasema: "Wakati watoto wanapokumbana na mzozo utokanao na kutosahamiliana, ujinga na ukosefu wa usawa, wanapaswa kufahamu namna ya kukabiliana na hali hiyo.  Kitabu hiki kina maelezo kwa msomaji Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu na kina wasililisha mazingira halisi. Kitabu hiki kunapaswa watoto fursa ya kuchunguza dhana walizokuwa nazo kuhusu wengine."

Kitabu hicho kimechapishwa Ujerumani mwaka 2021 na kinabainisha wazi madhara mabaya ya chuki dhidi ya Uislamu kwa mustakabali wa watoto.

Walengwa wakuu katika kitabu hicho cha kurasa 32 ni watoto walio na umria wa miaka 10-14.

Uchunguzi ulifanywa na Idara ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Ujerumani kwa kushirikiana an Wizara ya Mambo ya ndani ya Ujerumani chini ya anwani isemayo: "Maisha ya Waislamu nchini Ujerumani mwaka 2020" unaonyesha kuwa, kuna Waislamu milioni 5.3 hadi milioni 5.6 nchini humo na kwamba kiasi hicho ni sawa na asilimia 6.4 hadi 6.7 ya jamii yote ya Wajerumani.

Utafiti huo unasema idadi ya Waislamu nchini Ujerumani imeongezeka kwa watu laki tisa ikilinganishwa na matokeo ya uchunguzi uliofanyika mwaka 2015.

Idadi ya Waislamu wenye asili ya Uturuki nchini Ujerumani inafikia milioni 2.5 sawa na asilimia 45 ya Waislamu wote wa nchi hiyo.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa Waislamu milioni 1.5 wa Ujerumani waliwasili nchini humo kutokea katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiarabu wakiwemo asilimia 19 kutoka Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.

4010401

captcha